UTATA MANISPAA YA ILALA: SERIKALI YAPINGA KUAPISHWA KWA VIONGOZI!!


Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Migombani-Segera, Japhet Albert Kembo akiapishwa jana jijini Dar es Salam.
Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ilala amepinga vikali  kuapishwa kwa mwenyekiti wa mtaa wa segera-Migombani kulikofanywa na wakili binafsi, akisema kuwa ni ubabaishaji na kitendo ambacho hakikubaliki kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi. 
Kauli hii imekuja Siku moja baada ya wananchi wa mtaa huo wa Migombani jijini Dar es Salaam kuchukua dhamana ya kumuapisha mwenyekiti wao kwa kutumia wakili binafsi.

Wakati Mkurugenzi huyo wa Ilala akitoa kauli hiyo, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimbo la Segerea, Gango Filemon Kidera amebainisha kuwa wananchi wataendelea kupata huduma za kiserikali kutoka ofisi hiyo kama inavyotakiwa kwani kilichofanywa kilikuwa wazi na kilizingatia sheria za nchi na si batili kama inavyozaniwa.

“Tunasubiri tuone mkurugenzi anataka kumuweka nani badala ya kiongozi ambaye wananchi wamemchagua. Sababu za kutowaapisha viongozi waliochaguliwa hazijitoshelezi ndiyo maana wananchi wameshinikiza zoezi hilo lifanywe na wakili wa kujitegemea na sheria zinaruhusu kwakuwa zinataka mtu anayefanya hivyo ama awe hakimu au kamishna wa viapo,” alisema Kidera.

Aidha aliendelea kwakusema kuwa “Endapo kutakuwa na utata wowote utakaojitokeza baada ya mwenyekiti na wajumbe wake kuanza kutekeleza majukumu yao basi nguvu ya umma itatumika kuamua hatma ya hali hiyo…tutaandamana na wananchi wanasubiri kuona hilo linatokea.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment