KURUGENZI ya
Mawasiliano ya Rais Ikulu Dar es Salaam, imesema Rais
Jakaya Mrisho Kikwete atatoa uamuzi wake juu ya Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo aliyewekwa kiporo baada ya kuhusishwa kwenye
sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mkurugenzi wa
Mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu aliyasema hayo Dar es Salam jana
wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa Rais
Kikwete atatoa uamuzi wake baada ya uchunguzi kukamilika.
Alisema pamoja na Bunge
kutoa maazimio yake ili yaweze kutekelezwa na mamlaka ya uteuzi,
taratibu za kumwajibishan mtumishi wa umma na kiongozi wa kisiasa
unatofautiana ndiyo maana Prof. Muhongo yupo hadi sasa.
Akizungumzia suala la
wabunge kukwerwa na misamaha ya kodi, Bw. Rweyemamu alisema hata Serikali
haipendezwi na jambo hilo kwani bila kukusanya kodi hakuna maendeleo.
"Misamaha hii
inawachukiza wabunge kwa sababu bado hawajapitisha sheria ya kuifuta
misamaha hiyo...mwaka 2014, Serikali ilipeleka Muswada wa Sheria bungeni
ili kuifuta misamaha yote ya kodi lakini wabunge walikataa kuipitisha.
"Nashangaa kuona baadhi
ya wabunge kukerwa na misamaha ya kodi wakati wao ndiyo waliokataa
kupitisha muswada wa kufuta misamaha hiyo bungeni," alisema Bw.
Rweyemamu.
Juzi Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliitaka Serikali ifanye kila
linalowezekana ili kupunguza misamaha ya kodi ambayo mwaka wa fedha
2013/14 ilipaa kwa sh. bilioni 340 kutoka sh.trilioni 1.48 hadi sh.
trilioni 1.82 mwaka 2014.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment