BEACH SOCCER: KENYA YAIFUNGA BURUNDI NCHINI TANZANIA!!



Timu ya mchangani kutoka Kenya (wanaume) imeifunga Burundi kwa seti 2-1 katika michuamo ya wavu ya ufukweni ya Kanda ya 5 kwa ajili ya
kufuzu kucheza michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwakani mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Katika michuano inayoendelea katika fukwe za Mbalamwezi jijini Dar es Salaam, Kenya waliwatala seti ya kwanza na kushinda 21-13.
Burundi, katika jitihada za kupata ushindi, walifanikiwa kushinda seti ya pili kwa pointi 21-14.
  Seti ya tatu ilikuwa na ushindani na Kenya walifanikiwa kupata pointi 15 dhidi ya 13 za wapinzani wao.

Katika mechi nyingine ya wanawake, Burundi walishinda kwa seti 2-1 Mechi kadha hadi mchezo huo kumalizika, Mchezo mwingine unatarajiwa kufanyika katika siku zijazo ambapo timu kadhaa zinaendelea Jumatano huku
wenyeji Tanzania wakicheza na Kenya katika upande wa wanaume.

Kenya (wanawake) watacheza na Tanzania. Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa wenyeji wa michuano ya kufuzu kucheza
Olimpiki.

Timu zinazoshiriki michuano hiyo ya Dar es Salaam ni Kenya, Burundi na Tanzania.
Timu zitakazoibukwa washindi kwa upande wa wanaume na wanawake zitashiriki katika michuano ya Afrika itakayofanyika Congo Brazzavile, hatua ya mwisho kabla
kuelekea Rio de Janeiro.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment