KIKOSIKAZI
cha FIFA kimependekeza kuwa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2022
zitakazochezwa Nchini Qatar zichezwe Mwezi Novemba na Desemba.
Sambamba
na hilo, pia imependekezwa kuwa Fainali hizo zifupishwe kwa sababu ya
kuziondoa muda wake wa kawaida wa Miezi ya Juni na Julai.
Sababu
kubwa ya Fainali hizo za Mwaka 2022 kupendekezwa kutochezwa Juni na
Julai ni kutokana na hali ya joto ambalo hufikia zaidi ya Nyuzijoto
Sentigredi 40 huko Qatar katika kipindi hicho.
Baada
ya Qatar kuteuliwa kuwa Mwenyeji wa Fainali za 2022 kuliibuka upinzani
mkubwa kuhusu uamuzi huo huku ikitajwa Joto kuwa kipingamizi licha ya
Nchi hiyo kusema iko tayari kutumia Teknolojia kwenye Viwanja ili kupoza
hali ya Hewa.
Ndipo
FIFA ilipoamua kuweka Kikosikazi ili kushauriana na Watangazaji,
Wadhamini, Wadau wengine na hasa Ligi kubwa za Soka Barani Ulaya.
Kufuatia mashauriano ya Miezi 6 Kikosikazi hicho kimetoa Mapendekezo yao baada ya Mkutano wao huko Doha, Qatar hii Leo.
Kamati Kuu ya FIFA, itakayokutana huko Zurich, Uswsisi hapo Machi 19 na 20 ndio itatoa uamuzi wa mwisho.
Home / MICHEZO
/ FAINALI KOMBE LA DUNIA 2022:KIKOSIKAZI FIFA CHAPENDEKEZA KUFANYIKA NOVEMBA, DESEMBA KUEPUKA JOTO!!
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment