![]() | |
Siku ya Jumanne Usiku zipo Mechi 4 na Siku ya Jumatano zipo Mechi 6.Katika mechi hizo
kwa siku ya Jumanne, Arsenal, ambao wapo Nafasi ya 6, wapo kwanye uwanja wao wa nyumbani Emirates kucheza na Leicester City ambayo iko mkiani ikishikilia Nafasi ya 20.
Mechi nyingine kali ya siku hiyo ya Jumanne ni ile ya kule Anfield wakati Liverpool, walio Nafasi ya 7, watakapo ikaribisha Tottenham ambayo iko Nafasi ya 5 ikiwa Pointi 4 mbele ya Liverpool.
Mechi za Jumatano Usiku ni pamoja na ile ya Vinara wa Ligi, Chelsea, watakaokuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Everton wakati kule Old Trafford, Manchester United, ambayo ipo Nafasi ya 4, itawakaribisha Burnley walio Nafasi ya 17.
Mabingwa Watetezi wa Ligi, Man City, wao watakuwa Wageni huko Britannia Stadium kucheza na Timu ngumu Stoke City.
Timu iliyo Nafasi ya 3, Southampton, wao wapo Nyumbani kwao Saint Mary’s kuivaa Timu kali Msimu huu, West Ham United.
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumanne Februari 10
2245 Arsenal v Leicester
2245 Hull v Aston Villa
2245 Sunderland v QPR
2300 Liverpool v Tottenham
Jumatano Februari 11
2245 Chelsea v Everton
2245 Man United v Burnley
2245 Southampton v West Ham
2245 Stoke v Man City
2300 Crystal Palace v Newcastle
2300 West Brom v Swansea
MSIMAMO:
![TEBO-BPL-FEB8](http://www.sokaintanzania.com/images/TEBO-BPL-FEB8.jpg)
0 comments:
Post a Comment