SERIKALI KUANGALIA UWEZEKANO WA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA NCHI KUPIGA KURA!!

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni leo Mjini Dodoma

Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema serikali inaangalia utaratibu utakaowawezesha watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. 

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo bungeni mjini DODOMA wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa baadhi ya wabunge waliotaka kujua maandalizi yaliyofanywa kuwawezesha watanzania hao watekeleze demokrasia yao kuchagua viongozi. 

Waziri Mkuu PINDA amesema suala la maandalizi ya uchaguzi yakiwemo ya kuwashirikisha watanzania waliopo nje linashughulikiwa na Tume ya Taifa ya Tanzania Bara -NEC na Tume ya Uchaguzi ZANZIBAR - ZEC.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment