Tukio hilo lililovuta hisia za wananchi wengi wa
wilaya hiyo na wadau wa tasnia ya sheria, lilitokea jana saa 10:00 jioni
katika baa moja iliyopo jirani na mahakama ya wilaya hiyo.
Habari za uhakika zilizopatikana leo na
kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa Takukuru, zilisema kabla ya mtego
huo, Hakimu huyo alikuwa amepokea Sh500,000 kwa M-Pesa.
Kwa mujibu wa habari hizo, Hakimu huyo aliomba
rushwa hiyo ili aweze kutoa dhamana kwa mtuhumiwa mmoja aliyekuwa
mahabusu katika gereza la Kiruru la wilayani Mwanga.
Jina la Hakimu huyo ambaye jana alihamishiwa mjini Moshi kwa mahojiano, tunalihifadhi kwa sasa kwa sababu za kimaadili.
“Kuna bwana yuko gerezani alishindwa kutimiza
masharti ya dhamana kwa hiyo mheshimiwa (Hakimu) akamwambia mkewe ampe
Sh500,000 ili ampatie dhamana,” kilidokeza chanzo chetu.
Mtoa habari huyo alidai, mke wa mtuhumiwa huyo
alimtumia Hakimu huyo Sh500,000 kwa njia ya M-Pesa lakini akashangaa
mumewe kutopewa dhamana na Hakimu huyo.
Inadaiwa badala yake, Hakimu huyo alitaka
aongezewe Sh500,000 nyingine na ndipo mke wa mtuhumiwa huyo alipotoa
taarifa Takukuru na mtego kuandaliwa.
Taarifa za kukamatwa kwa Hakimu huyo zilizagaa kwa
kasi kuanzia jana usiku huku wananchi wa kawaida na mahakimu
wakitumiana meseji wakihabarishana juu ya tukio hilo.
Jitihada za kumpata Kamanda wa Takukuru mkoa
Kilimanjaro, Lawrence Swema ili kuthibitisha au kukanusha tukio hizo,
hazikuzaa matunda kwani simu yale ilikuwa ikiita bila majibu na meseji
hazijibiwi.
Chanzo: Mwananchi
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment