Daladala zikiwa katika stendi ya Ubungo jijini Dar es Salaam tayari kupakia abiria. Picha na Maktaba |
Ushauri huo umekuja siku tatu tangu Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), kupunguza bei ya mafuta
kwa mara nyingine katika kipindi cha miezi mitatu, huku punguzo la sasa
likitajwa kuwa ni la chini zaidi katika kipindi cha miaka sita
iliyopita.
Katibu mtendaji wa baraza hilo, Dk Oscar Kikoyo
alisema kwa kuwa punguzo hilo limefikia Sh1,652 kwa petrol na Sh1,563
kwa dizeli, huku mafuta ya taa yakiuzwa Sh1,523, kuna haja ya mamlaka
hiyo kupunguza nauli za mabasi kwa asilimia 15 hadi 24.
“Katika ukokotoaji, ikiwa wamiliki wa mabasi
watapata faida ya asilimia 25 hadi 30, lazima nauli ishuke ili kuendana
na mtiririko uliopo ili kuleta mlingano ulio sawa,” alisema Dk Kikoyo na
kuongeza:
“Baada ya kuangalia mfumo wa ukokotoaji,
tumependekeza kwa Sumatra ishushe nauli kwa mlingano wa asilimia 15-24.
Kwa hiyo, nauli za daladala zishuke kwa Sh50, huku mikoani mfano Dar
mpaka Arusha ishuke kutoka Sh36,000 mpaka Sh28,000.”
Dk Kikoyo alisema kuwa baraza limekuwa likikusanya
takwimu tangu kushuka kwa bei mwishoni mwa mwaka jana na kuendelea na
ukokotoaji.
“Tumeangalia mambo mengi kwani licha ya mafuta
kushuka bei, vipuri vya magari vipo juu. Lakini tunaamini kushuka nauli
kutaleta tija kwa mtumiaji, maana kuna wengine wanashindwa kusafiri
kutokana na gharama kuwa juu,” alisema Dk Kikoyo.
Hii ni mara ya pili mafuta kushuka bei hadi
kufikia Sh1,652. Awali, iliwahi kutokea Mei mwaka 2009, ambapo bei ya
petroli ilishuka kutoka Sh2,200 hadi Sh1,147 na ikapanda tena kwa hadi
kufikia Sh2,000 na zaidi. Baada ya hapo haikuwahi kushuka hadi mwishoni
mwa mwaka jana iliposhuka kwa Sh1,768.
0 comments:
Post a Comment