MCT yavipa muda vyuo vya uandishi wa habari

 

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limevitaka Vyuo vyote vya Uandishi wa Habari Tanzania ambavyo vimepewa muda wa kukidhi vigezo vinavyotakiwa ili kutumia mitaala mipya katika kiwango kinachotakiwa, vifanye hivyo kabla ya kufanya ukaguzi mwingine mapema mwakani.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alipotoa taarifa kuhusu ukaguzi waliofanywa na MCT kwa kushirikiana na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari nchini.

“MCT kwa kushirikiana na NACTE, tulifanya ukaguzi wa vyuo nchini na kugundua vyuo vingi vya uandishi wa habari havijakidhi mahitaji ya mitaala ya kufundishia.

“Ukaguzi huo ulibainisha mpaka sasa kuna vyuo viwili vilivyofanikiwa kukidhi vigezo vyote muhimu vinavyotakiwa na vimeruhusiwa kutumia mitaala hiyo ambavyo ni A3 Institute of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam na Arusha Journalism Training College cha jijini Arusha.

Mukajanga alisema, vyuo vilivyopewa muda wa kukidhi vigezo ni Dar es Salaam School of Journalism (DSJ),Time School of Journalism (TSJ) na Royal College of Tanzania (RCT) vya jijini Dar es Salaam, pamoja na Institute of Social and Media Studies cha Arusha na Zanzibar Journalism and Mass Media College cha Zanzibar.

Chuo cha City Media College kilichopo jijini Arusha kilichoruhusiwa kutumia mitaala ya zamani tangu mwaka jana kimefungwa, baada ya kushindwa kukidhi vigezo na kimebainika kuwa kimerudi nyuma katika kukidhi vigezo tangu ukaguzi uliopita.

Kwa vyuo vinavyoruhusiwa kutumia mitaala kwa muda vitapofanyiwa ukaguzi wa mara ya pili na kuonekana kuwa vinakidhi vigezo vyote muhimu, huruhusiwa kutumia mitaala papo hapo.

Alisema kwa vile vyuo ambavyo vinaonekana vimefanya jitihada lakini bado havijakidhi vigezo huongezewa muda na chuo kitakachoonekana kuwa hakifanyi jitihada za kuboresha mitaala hufugwa kabisa.

Pia kuna vyuo vitatu ambavyo vimeruhusiwa kutumia mitaala ya taifa ya kufundishia ni pamoja na EMAGS College of Art and Media, Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro na Kyela Polytechnic.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment