Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Paul Kagame wa Rwanda wakati walipokutana faragha sambamba na mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliofanyika katika Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala,Uganda, leo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika mazungumzo na Marais Paul
Kagame wa Rwanda(kushoto), Rais Salva Kiir wa Sudan ya kusini na Rais
Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda
Baadhi
ya viongozi wan chi za jumuiya ya Maziwa Makuu wakiwa katika picha ya
pamoja wakati wa Mkutano wa wakuu wa nchi hizo uliofanyika jijini
Kampala Uganda leo.Kutoka kushoto ni Rais Salva Kiir wa Sudani ya
Kusini,Rais Joseph Kabila wa DRC,Rais Dkt.Jakaya Kikwete,Rais Yoweri
Museveni wa Uganda,Mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika
Dkt.Nkosazana Dlamini Zuma na Rais Paul Kagame wa Rwanda.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais Paul Kagame
wa Rwanda wakati walipokutana na kufanya mazungumzo ya faragha, katika
Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, jijini Kampala
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani.
Viongozi
hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika
kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa
Kampala, Uganda.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea
kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati
ya nchi hizo mbili.
Viongozi
hao wawili wako nchini Uganda kuhudhuria Mkutano wa Nchi Wanachama wa
Umoja wa Kimataifa wa Maziwa Makuu – “International Conference on the
Great Lakes Region (ICGLR)” unaofanyika leo Hoteli ya Munyonyo
Commonwealth Resort.
Viongozi
wengine ambao wanahudhuria Mkutano huo ni pamoja na Rais Yoweri
Museveni wa Uganda ambaye ni Mwenyekiti wa ICGLR na mwenyeji wa Mkutano
huo, Rais Silva Kiir wa Sudan Kusini, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika (AU).
Rais
Kikwete na ujumbe wake amewasili Kampala asubuhi ya leo akitokea mjini
Dodoma ambako aliwasili jana jioni kwa ajili ya hafla ya kuwaapisha
Makatibu Wakuu watatu na Naibu Makatibu Wakuuu wawili iliyofanyika Ikulu
Ndogo, Dodoma.
Rais
Kikwete aliwasili Dodoma akitokea Mwanza ambako alihudhuria mazishi ya
Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania
(EAGT) Askofu Mkuu Dkt. Moses Samwel Kulola yaliyofanyika kwenye Kanisa
la Bugando Calvary Temple, mjini Mwanza.
0 comments:
Post a Comment