Viongozi wa Afrika waliokuwa wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia,
wamekubaliana kuwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya asihudhurie kesi yake
katika Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ila ikiwa itaakhirishwa.
Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema kuwa kiongozi yeyote wa
taifa asitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya kimataifa wakati yuko
madarakani.
Bwana Kenyatta siku zote amesema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.Kesi ya Rais Kenyatta ambaye anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu inatarajiwa kuanza mwezi ujao mjini Hague, ingawa ameomba mara kadha kwamba iakhirishwe.
AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, alisema kesi
za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar al-Bashir wa Sudan zinaweza
kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano katika nchi zao.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment