
Meneja wa Cardiff City, Malky Mackay,
ambae leo Timu yake imechapwa Bao 4-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England
licha ya kuongoza kwa Bao 1-0, amemlaumu Refa Anthony Taylor kwa kufanya
uamuzi uliobadilisha Gemu yao hiyo.
Jordon Mutch alitangulia kuipa Bao
Cardiff City lakini Chelsea walijibu katika Dakika ya 33 baada ya Kipa
wa Cardiff City, David Marshall, aliekuwa amaedaka Mpira, kuudunda Mpira
chini na Samuel Eto’o kuudokoa na baadae kumfikia Hazard aliefunga
lakini Wachambuzi wamebainisha kuwa Kisheria Goli hilo lingetakiwa
kutokubaliwa.
Ingawa Chelsea waliongeza Bao 3 zaidi
baada ya Bao hilo, lakini Meneja Malky Mackay anaamini makosa ya Refa
Anthony Taylor kulikubali Bao hilo la kusawazisha ndio limewaua.
Alisema: “Ilitakiwa kuwa ni faulo lakini imewapa Goli na tumekwenda Haftaimu 1-1 badala ya sisi kuwa 1-0 mbele. Ni kosa kubwa!”
Baada ya Mechi Mackay aliiambia Sky
Sports: “Nilikwenda kuongea na Refa kutaka kujua nini kimetokea
akaruhusu Bao lile. Refa Msaidizi alidhani Kipa aliuweka Mpira chini!
Nikamuuliza kama kaudunda je? Akajibu kama aliudunda sio Goli ni faulo
lakini sie tulijua kauweka chini!”
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment