KIZAAZAA UWANJA WA TAIFA LEO SAA KUMI JIONI!!


DABI_YA_KARIAKOOLEO ndio ule Mtanange Spesho, uliobatizwa Jina la ‘DABI ya KARIAKOO’, unaozikutanisha Yanga na Simba, Klabu za Eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam ambao ni Wapinzani wa Jadi.

Hii ni Mechi ya kwanza kati yao ya VPL, Ligi Kuu Vodacom na Simba wapo kileleni mwa Ligi hiyo kwa kushinda Mechi 5 na Sare 3 wakiwa na Pointi 18 wakati Yanga wameshinda Mechi 4 Sare 3 na kufungwa 1 na wana Pointi 15.
Simba, ambao wako chini ya Kocha Abdallah Kibaden, walikuwa mafichoni huko Bamba Beach, Kigamboni, Dar es Salaam wakinoa Mfumo wao wa 4-4-2 ambao wanatarajiwa kuutumia leo hii.
Yanga, chini ya Kocha Ernie Brandts kutoka Holland, wao walijichimbia Visiwani Pemba, wakjizoeza na Fomesheni yao ya 4-3-3 ambayo huwafanya washambulie muda wote.

REKODI:
LIGI KUU: Ushindi Yanga 37 Simba 32 Sare 31
UBINGWA: Yanga 23 Simba 18

Wakiongea kabla Mechi hii, Kocha wa Simba, Kibaden, ameripotiwa kutamka kuwa Timu yake imejitayarisha vyema na ipo kwenye hali ya ushindi.
Nae Brandts wa Yanga amesema Wachezaji wake wote wako fiti na wako tayari kuwavaa wapinzani wao.

DONDOO MUHIMU:
-BEI ZA TIKETI:
-Sh. 5,000 Viti vya rangi ya kijani [Viti 19,648]
-Sh 7,000 Viti vya rangi ya bluu
-Sh 10,000 Viti vya rangi ya chungwa 
-Sh 15,000 VIP C
-Sh 20,000 VIP B
-Sh 30,000 VIP A [Viti 748]
-TIKETI KUUZWA SIKU MOJA.
-VITUO MAUZO YA TIKETI: Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
-REFA: Israel Nkongo [Dar es Salaam] 
-MAREFA WASAIDIZI: Hamis Changwalu [Dar es Salaam] na Ferdinand Chacha [Bukoba]
-REFA wa AKIBA: Oden Mbaga [Dar es Salaam].
-KAMISHNA: John Kiteve [Iringa] 
-MTATHMINI WA WAAMUZI: Stanley Lugenge [Njombe]

Mara ya mwisho Timu hizi kukutana ni hapo Mei 18 katika Mechi ya mwisho ya Msimu wa VPL wa 2012/13, Msimu ambao Yanga aliibuka Bingwa, na katika Mechi hiyo Simba alinyukwa Bao 2-0 kwa Bao zilizofungwa na Didier Kavumbagu na Hamisi Kiiza.
Katika Mechi hiyo, Supastraika, Mrisho Ngassa, alivaa Jezi ya Simba lakini safari hii, Ngassa atavaa Jezi ya Yanga.

VPL: MECHI ZA YANGA NA SIMBA LIGI MSIMU HUU 2013/14
YANGA
P:8 W:4  D: 3 L: 1
SIMBA
P: 8 W:5 D:3 L:0
Yanga 5 Ashanti 1

Rhino Rangers 2 Simba 2

Yanga 1 Coastal Union 1

JKT Oljoro 0 Simba 1

Mbeya City 1 Yanga 1

Simba 2 Mtibwa Sugar 0

Tanzania Prisons 1 Yanga 1

Simba 6 Mgambo JKT 0

Azam FC 3 Yanga 2

Simba 2 Mbeya City 2

Yanga 1 Ruvu Shooting 0

JKT Ruvu 0 Simba 2

Yanga 2 Mtibwa Sugar 0

Ruvu Shooting 1 Simba 1

Kagera Sugar 1 Yanga 2

Simba 1 Tanzania Prisons 0


VIKOSI VINAWEZA KUWA:
YANGA [Mfumo 4-3-3]: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Athuman Idd 'Chuji', Haruna Niyonzima, Frank Domayo 'Chumvi' , Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa, Hamis Kiiza.

SIMBA [Mfumo 4-4-2]: Abel Dhaira, Nassor Said, Rashid Issa, Kaze Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Abdulhalim Humuod, Ramadhan Singano, Haroun Chanongo, Amisi Tambwe, Betram Mombeki.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment