WATANZANIA KUKUMBUKA KIFO CHA MWALIMU NYERERE KESHO,NA HII NI SEHEMU YA HISTORIA YAKE KWAUFUPI.



Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere.
WAKATI Taifa linaadhimisha kifo cha mwasisi wa Taifa la Tanzania, na Rais wa kwanza wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kila mwaka ifikapo tarehe 14/10, kizazi hiki kinahitaji kujua huyo alikuwa mtu gani na alianzia wapi.

katika makala haya, tutaangalia sehemu tu ya historia ya mwalimu, nia ni kutaka kumuezi na kujikumbusha kama huyu tunayemuenzi leo alikuwa mtu gani na jinsi alivyoishi.


Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa ni mmoja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila kitu ya Nyerere, Mapadre wa Kanisa katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri ya kutaika kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.akiwa katika Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia akaamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s), Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya.

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                 aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

 Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.

Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu. Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu.

Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu Justine Samba.

Alikuwa mwanamichezo
Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wan chi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo, aliazznisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama alicheza bao nyumbgani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.

Kutokana na maisha yake aliyoyaishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini hasa kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Taifa linamkumbuka kwa hayo na mengi ambayo aliyafanya, ameacha machapisho mengi ambayo pia yamekuwa hazina ya maarifa kwa watanzania
Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA)
@Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment