WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI IMERIDHIA KUONGEZWA MUDA KWA WANAFUNZI 1,107 WENYE VIGEZO VYA KUPATIWA MKOPO.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imeridhia kuongezwa kwa muda kwa wanafunzi 1107 wenye vigezo vya kupatiwa mikopo waliokosea kujaza fomu za kuomba mikopo hiyo kutoka Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi PHILIP MULUGO amesema wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii kuwa, wanafunzi hao ni wale walioomba kwenye fani za Hisabati wanafunzi 20, Ualimu wa Sayansi Wanafunzi 164, Sayansi ya Tiba 111, Uhandisi Umwagiliaji Saba, Ualimu 617, Sayansi ya Kilimo 20, Uhandisi 70 na Sayansi 98.
Naibu Waziri MULUGO amesema jumla ya shilingi Bilioni 1.9 zinahitajika kwaajili ya Chakula na Malazi, shilingi milioni 221.4 kwaajili ya Vitabu na Viandikwa, Shilingi milioni 686.3 kwaajili ya Mafunzo kwa Vitendo na milioni 221.4 kwaajili ya Mahitaji Maalum ya Vitivo ambapo Wizara itaandika barua vyuoni kuomba wanafunzi hao wasome kwa mkopo hatua ambayo imepongezwa na kamati kupitia kwa mwenyekiti wake MARGARET SITTA.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo kupitia kwa makamu wake STEVEN NGONYANI Mbunge wa Korogwe vijijini imeshtushwa na taarifa iliyowasilishwa na Wizara ya Elimu kuhusu uwepo wa vyuo 46 nchini ambavyo vinatoa elimu bila ya kuwa na usajili wa NACTE ambapo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo SIFUNI MCHOME amesema tayari wameviandikia barua vyuo hivyo.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment