TIMU YA ARSENAL HAWAJASHINDA KATIKAUWANJA WA OLD TRAFFORD TANGU 2006!!
MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema
Mechi yao ya Jumapili huko Old Trafford na Manchester United
‘itashangaza’ kwa kutokuwepo Sir Alex Ferguson.
Ferguson na Wenger ndio walikuwa
Mameneja waliotumikia Ligi Kuu England kwa muda mrefu kabla Sir Alex
Ferguson hajaamua kustaafu Mwezi Mei.
Timu hizi zilishakutana USO kwa USO mara 175 matokeo yake yakawa hivi,
Man United ikawa imeibuka na Ushindi mara 75 huku Arsenal ikiwa na Ushindi mara 60 wakati huo Sare zikiwa mara 40.
Arsenal,
ambayo ndio inaongoza Ligi, inaweza kuwa Pointi 11 mbele ya Man United
ikiwa itashinda Mechi hiyo lakini Wenger amesema ni mapema mno kuanza
kumpima mrithi wa Ferguson, David Moyes alietokea Everton.
Wenger amesema: “Ni ajabu bila Ferguson
kuwepo Siku ya Jumapili. David Moyes ameonyesha kazi nzuri huko Everton
na inabidi umwachie ajijenge na Man United na sasa polepole anafa hivyo.
Utaona matokeo yake ya sasa! Ikitokea Mtu kakaa sehemu Miaka 26 na
kuondoka, inachukua muda kwa Mtu mpya. Ni ngumu na hatari kwa Meneja
mpya. Kwangu mimi, Moyes anafanya kazi nzuri.”
Wenger na Ferguson walikuwa na upinzani mkubwa na upo wakati, Mwaka 2005, waliombwa kumaliza uhasama wao na Polisi.
Hilo lilitokea mara baada ya Man United
kuifunga Arsenal Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford na kumaliza mbio za
Arsenal za kutofungwa katika Mechi 49 za Ligi kisha Wachezaji wa Arsenal
wakaripotiwa kumrushia Ferguson Pizza.
Arsenal hawajaifunga Man United Uwanjani
Old Trafford tangu Mwaka 2006 na wamekuwa wakifungwa katika kila Mechi
ya Mechi zao 5 zilizopita ikiwemo kisago cha Bao 8-2 Agosti 2011.
ARSENAL UWANJANI OLD TRAFFORD TANGU 2006:
3 Novemba 2012: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
28 Agosti 2011: Man United 8-2 Arsenal (Ligi Kuu)
12 Machi 2011: Man United 2-0 Arsenal (FA Cup)
13 Desemba 2010: Man United 1-0 Arsenal (Ligi Kuu)
29 Agosti 2009: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
16 Mei 2009: Man United 0-0 Arsenal (Ligi Kuu)
29 Aprili 2009: Man United 1-0 Arsenal (UEFA Championz Ligi)
13 Aprili 2008: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
16 Februari 2008: Man United 4-0 Arsenal (FA Cup)
Lakini safari hii Arsenal ni Vinara wa Ligi na wana Pointi 25 kwa Mechi zao 10 za Ligi wakiwa Pointi 5 mbele kileleni na hawajafungwa katika Mechi zao 14 kati ya 15 za Ugenini.
Ushindi wao wa mwisho umekuja Jumatano
huko Germany walipoifunga Borussia Dortmund Bao 1-0 kwenye Mechi ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI na Wenger anaamini Mechi yao hii ya Old Trafford ni moja
ya Mechi zao ngumu.
Wenger amesema: “Hii ni moja ya zile
Gemu ambazo zinakufanya ujenge imani na kupata mafanikio ukishinda. Hivi
karibuni hatujafanya vizuri Uwanja ule. Kitu muhimu ni kuamini uchezaji
wetu na umahiri wetu. Ni nafasi nzuri kuonyesha sasa tuna mafanikio.”
Alieuwa Nahodha wa Arsenal, Robin van
Persie, kabla kuhamia Man United Mwezi Agosti Mwaka 2012 na kuifungia
Bao 26 zilizoisaidia kuipa Ubingwa, anatarajiwa kuivaa Klabu yake ya
zamani kwa mara ya tatu hapo Jumapili na Wenger anaamini ni kazi ya
aliekuwa Kocha Man United, Rene Meulensteen, anaetoka Holland, ndie
aliemshawishi Van Persie kujiunga na Man United.
RATIBA YA BPL: LIGI KUU ENGLAND WEEK END HII;
Jumamosi Novemba 9
18:00 Aston Villa v Cardiff
18:00 Chelsea v West Brom
18:00 Crystal Palace v Everton
18:00 Liverpool v Fulham
18:00 Southampton v Hull
20:30 Norwich v West Ham
Jumapili Novemba 10
15:00 Tottenham v Newcastle
17:05 Sunderland v Man City
19:10 Man United v Arsenal
19:10 Swansea v Stoke
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
10 |
13 |
25 |
2 |
Chelsea |
10 |
8 |
20 |
3 |
Liverpool |
10 |
7 |
20 |
4 |
Tottenham |
10 |
4 |
20 |
5 |
Man City |
10 |
17 |
19 |
6 |
Southampton |
10 |
7 |
19 |
7 |
Everton |
10 |
4 |
19 |
8 |
Man United |
10 |
4 |
17 |
9 |
Newcastle |
10 |
-2 |
14 |
10 |
Hull |
10 |
-2 |
14 |
11 |
West Brom |
10 |
0 |
13 |
12 |
Cardiff |
10 |
-4 |
12 |
13 |
Swansea |
10 |
0 |
11 |
14 |
Aston Villa |
10 |
-3 |
11 |
15 |
West Ham |
10 |
0 |
10 |
16 |
Fulham |
10 |
-5 |
10 |
17 |
Stoke |
10 |
-4 |
9 |
18 |
Norwich |
10 |
-14 |
8 |
19 |
Sunderland |
10 |
-15 |
4 |
20 |
Crystal Palace |
10 |
-15 |
3 |
0 comments:
Post a Comment