MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA) YASEMA WATENDAJI WATAKAODAI FEDHA ZA VITAMBULISHO KUKIONA!!


NIDA1 a9f58
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaonya baadhi ya watendaji wa mitaa jijini Dar es Salaam wanaodaiwa kuwatoza fedha wananchi kwa ajili ya kuwapatia vitambulisho hivyo na kwamba wakibainika watachukuliwa hatua za sheria.

Aidha, imesema zoezi la utaoji wa vitambulisho limefikia katika hatua ya kuchukua alama za vidole na picha kwa watu waliojaza fomu za kuviomba.
Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Dickson Maimu, akizungumza katika mahojiano na Radio One, alisema zoezi la vitambulisho linagharamiwa na serikali kwa asilimia 100, hivyo hairuhusiwi mtendaji yeyote kumtoza fedha mwananchi.
Alisema zoezi linaendelea katika wilaya za Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar na kuwa wanaopuuza kupata vitambulisho vya taifa watapata athari ikiwamo kushindwa kupata huduma mbalimbali kama kufungua akaunti au kupata ajira.
Kuna madai kuwa baadhi ya watendaji wa mitaa katika jijini Dar es Salaam wamekuwa wakiwatoza Sh. 2,000 watu wanaokwenda katika ofisi zao ili kugongewa mihuli.
CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment