MAHAFALI YA SABA KATIKA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (AJTC) KUFANYIKA HIVI KARIBUNI!!



Maafali ya saba katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) yanatarajiwa kufanyika hivi  kwa na lengo la kuwaaga wanafunzi wanaohitimu ngazi ya Cheti na Stashahada katika tasnia ya habari.

Kwa mujibu wa  Mlezi wa wanafunzi wa chuo hicho Bw.Andrew Ngobole alisema kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo anatarajiwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh.Nyirenda Munasa. 


 Mahafali hayo yanatarajia kufanyika mnamo tarehe sita (6) mwezi wa kumi na mbili katika ukumbi wa PPS ulioko maeneo ya Mbauda mkoani Arusha ikiwa ni mahafali ya saba tangu kuanzishwa kwa chuo hicho.

Aidha Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji (AJTC) kimekuwa na desturi yakuwapatia  wanafunzi waliofanya vizuri zawadi mbalimbali wakiwepo wale wote waliofanya vizuri katika masomo yao kinadharia na vitendo pamoja na walioonyesha nidhamu nzuri katika kila sekta kila mara maafali yanapofanyika.

Nae  Rais wa serikali ya wanafunzi katika Chuo hicho Bw.George Silange alisema Serikali yake inabaki na pengo kubwa kwani viongozi wanaoondoka ni wengi na waadilifu tena wachapakazi.

Pengo hilo linakuja mara tu baada ya viongozi sita wa serikali iliopo madarakani kuhitimu, hivyo kuwataka viongozi wanaobaki kufanya kazi kwa ushirikiano mpaka hapo atakapoteuwa viongozi watakaochukuwa nafasi hizo.

Amewataja viongozi hao kuwa nipamoja na Waziri wa elimu Bw.Denis  Kanzenzele, Waziri wa Habari Bw.Ndalike Saidi Sonda, Waziri wa fedha Bi.Patrokill Kamasho, Naibu waziri wa afya na makazi Bi.Jorida Faustin, Naibu waziri wa Michezo Bw. Emmanuel Chindiye, pamoja na Naibu Waziri wa ulinzi Bw.Kefas Daniel.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wanaohitimu waziri wa elimu Bw.denis Kanzenzele amesema “inatulazimu kuondoka kutokana na muda wetu kwisha ila ni majonzi mazito tuliyonayo mioyoni kuagana na Waalimu, viongozi wenzetu pamoja na wanafunzi wenzetu kutokana na mazoea tuliyokuwa nao pamoja na ushirikiano mkubwa tuliopata kutoka kwao”alisema Kanzenzele.

Aidha Bw.Kanzenzele aliwataka radhi  wanafunzi wanaobaki pale mahali walipowakosea, kisha kuahidi kuitumia vyema taaluma waliyoipata Chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na kuitangaza vyema AJTC popote waendapo.

Written by: Virginia Daniel.
Edited by:Emanueli Onesmo Ndanshau
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment