MNYIKA AWASILISHA HOJA BINAFSI KUHUSU KUCHUKA KWA KIWANGO CHA ELIMU NCHINI!!


Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amewasilisha hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, kuhusu kuporomoka kwa viwango vya ufaulu nchini akitaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, kuwajibika kuwasilisha bungeni ripoti ya tume/timu iliyoundwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Aidha amewasilisha hoja nyingine kuhusu gharama za maisha ambayo pamoja na mambo mengi atawabana mawaziri mizigo waweze kuachia ngazi.
Akithibitisha kwa NIPASHE kwa njia ya ujumbe mfupi jana,  Mnyika, alisema ametumia Kanuni ya Bunge ya kifungu cha 28 (9) kuwasilisha hoja hiyo ambayo inakataa waziri kuwajibika kutoa (majibu) taarifa hiyo bungeni.

“Kuna taarifa ya hoja nimewasilisha kuhusu gharama za maisha na ambayo pamoja na mambo mengine nitawabana mawaziri mizigo,” alisema.

Baada ya matokeo ya kidato cha nne mwaka jana kutangazwa na kuonekana kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiasi kikubwa, Waziri Mkuu Pinda aliunda timu/tume ya kuchunguza matokeo hayo na elimu kwa ujumla lakini ripoti hiyo baada ya kukamilika haijawekwa hadharani.

“Waziri awajibike kufuatia yeye mwenyewe na watendaji wenzake kusababisha udhaifu huo…katika maelezo (hoja) hayo nimekosoa pia kauli iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, katika mkutano uliopita wa Bunge kuhusu viwango na madaraja ya ufaulu ambao alificha udhaifu na ukweli ulioko ndani ya wizara ambao nina taarifa zake na uozo mwingine uliobainishwa na ripoti ya Pinda,” alisema.

POSTED BY:info@dirayetu.blogspot.com
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment