MOYES AJIPA MOYO UBINGWA, MOURINHO AUNGAMA KUWA WAKO MATATANI!!


MOYES_v_MOURINHOWAKATI David Moyes akijipa moyo kwa kusisitiza Manchester United bado wamo kwenye mbio za Ubingwa licha ya kushindiliwa vipigo viwili mfululizo Nyumbani kwao ndani ya Siku 4, Jose Mourinho ameungama kuwa Chelsea ipo matatani baada Jana kunyukwa Bao 3-2 na Stoke City huko Britannica Stadium.


DAVID MOYES ASEMA: MAN UNITED WANAWEZA KUTWAA UBINGWA!
Wamepokea vipigo viwili mfululizo ndani ya Siku 4 wakiwa kwao Old Trafford kitu ambacho hakijatokea tangu 2002 na wapo Pointi 12 nyuma ya Vinara Arsenal ambao wanacheza leo na Everton na pengo hilo linaweza kuwa Pointi 15 wakishinda leo, lakini Meneja wa Mabingwa Manchester United, David Moyes, amesisitiza bada nafasi ya kutwaa Ubingwa ipo.
Ametamka: “Nasimama imara nikiamini tutakuwa karibu. Natumai tutakuwepo kwenye kinyang’anyiro mwishoni mwa Msimu!”

MAN UNITED==ZINAZOFUATA:
10 Des
Man Utd v Shakhtar
UCL
15 Des
Aston Villa v Man Utd
LKE
18 Des
Stoke v Man Utd
LC
21 Des
Man Utd v West Ham
LKE
26 Des
Hull v Man Utd
LKE
28 Des
Norwich v Man Utd
LKE
1 JAN
Man Utd v Tottenham
LKE

Alipohojiwa kwanini ana imani kubwa kiasi hicho alijibu: “Wachezaji-nafanya kazi na Mabingwa!”
Jumatano iliyopita, Man United ilitunguliwa Bao 1-0 na Everton na Jana Newcastle pia walishindiliwa 1-0.
Moyes ameeleza: “Gemu ile na Everton na hii na Newcastle ziko sawa na kama tungeshinda hakuna Mtu angehoji. Hatukushinda, na kwa sababu sisi ni Manchester United, ni lazima tufanye vyema. Lazima tucheze vizuri zaidi, tuwe na pasi bora na tutumie nafasi zetu vizuri.”
JOSE MOURINHO AKIRI CHELSEA IKO MATATANI!
Jose Mourinho amesema Chelsea iko matatani baada ya kuumwaga uongozi wa Bao 1-0 na kuchapwa Bao 3-2 hapo Jana walipocheza na Stoke City.
Akionyesha kuwa na hasira, Jose Mourinho, mara baada ya kipigo hicho, alisema: “Sijisikii vizuri kiasi cha kuelezea Gemu ilikuwaje. Tupo matatani. Inasumbua kuona jinsi tunavyofungwa Magoli namna hii. Sipendi, na mimi sitayarishi Timu yangu iwe hivi.”
Kwa mara ya kwanza tangu Kipindi cha Aprili hadi Mei 1998, Chelsea imeruhusu kufungwa Bao 3 au zaidi katika Mechi mfululizo za Ligi Kuu England.
Katika Mechi zao 3 zilizopita dhidi ya Stoke, Sunderland  na Southampton, Chelsea imeruhusu Bao 7.

CHELSEA-MECHI ZINAZOFUATA: 
11 Des
Chelsea v Steau
UCL
14 Des
Chelsea v Palace
LC
17 Des
Sunderland v Chelsea
LKE
23 Des
Arsenal v Chelsea
LKE
26 Des
Chelsea v Swansea
LKE
29 Des
Chelsea v Liverpool
LKE
1 Jan
S’mpton v Chelsea
LKE

Chelsea sasa wako Nafasi ya 3 wakiwa wamefungana Pointi na Liverpool ambao wako Nafasi ya Pili kwa ubora wa Magoli na wote wako nyuma ya Vinara Arsenal kwa Pointi 4 lakini Arsenal watakuwa Pointi 7 mbele ikiwa wataifunga Everton baadae leo.
Hilo halikumteteresha Mourinho ambae amedai: “Ukitutizama sisi na kutulinganisha na Man City, Man Utd, Tottenham, Liverpool….sidhani kama tunafanya vibaya! ”
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA YA LEO
Jumatatu Desemba 9
2300 Swansea v Hull
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
14
19
34
2
Liverpool
15
16
30
3
Chelsea
15
13
30
4
Man City
15
26
29
5
Everton
14
9
27
6
Tottenham
15
-1
27
7
Newcastle
15
-1
26
8
Southampton
15
5
23
9
Man Utd
15
3
22
10
Aston Villa
14
0
19
11
Swansea
14
1
18
12
Stoke
15
-5
17
13
Hull
14
-6
17
14
Norwich
15
-14
17
15
West Brom
15
-4
15
16
Cardiff
15
-11
14
17
West Ham
15
-6
13
18
Crystal Palace
15
-12
13
19
Fulham
14
-14
10
20
Sunderland
15
-18
8

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment