Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi, imesema kuwa serikali ya Syria na waasi wamekubaliana kuruhusu msaada wa kibinaadamu kuingizwa mjini Homs.
Kiongozi wa waasi wa Syria Bw.Ahmed Assi al-Dscharba.
Msemaji wa wizara hiyo Alexander Lukashevich aliwaambia waandishi habari mjini Moscow, kuwa yaonekana makubaliano hayo yamefikiwa.
Maelezo yake yamekuja baada ya ujumbe wa Urusi katika Umoja wa Mataifa, kusema kuwa unapinga azimio la Baraza la Usalama kuhusu hali ya kibinaadamu nchini Syria.
Waasi wa Syria wakijiandaa kwenda kwenye mashambulizi
Chanzo DW
0 comments:
Post a Comment