Baada ya Rasimu mpya ya katiba ya kwanza kukakamilika katika chuo cha
Uandishi wa Habari na
Utangazaji Arusha(A.J.T.C) wanafunzi waunga mkono wakati wa maswali ya
papo kwa hapo yaliyokuwa yakiulizwa na wanafunzi na kujibiwa na
mwenyekiti wa tume ya katiba hiyo Bw Oscar Samba.
Mlezi wa wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha Bw Andrea Ngobole akipokea rasimu ya katiba kutoka kwa mwenyekiti wa tume ya katiba Bw Oscar Samba. |
Akitoa
ufafanuzi juu ya rasmu hiyo Mwenyekiti wa tume hiyo Bw.Oscar Samba alisema
kuwa ni wajibu wa kila mwanafunzi kutoa na kuchangia maoni katika
mchakato wa kutafuta katiba mpya.
Aidha
aliendelea kusema kuwa kila mwanafunzi anapaswa kutoa ushirikiano
wakati wakuchambua rasimu hiyo ili kujenga katiba iliyo bora na yenye
kusimamia haki , jinsia na usawa kwa wanafunzi wakati wakiwa masomoni.
Hata
hivyo Bw Oscar Samba alisema kuwa kupitia mapendekezo yaliyotolewa
kwenye rasmu hiyo ya katiba yanaeleza kuwa Waziri wa katiba na sheria
ndiye mwenye mamlaka ya kutoa adhabu kulingana na katiba itakavyo
ainisha na sio waziri wa nidhamu kama ilivyo awali.
Mchakato
wa rasimu ya katiba katika Chuo cha uandishi wa Habari na Utangazaji
Arusha ulianza rasmi mwishoni mwa mwaka jana mwezi wa october ukiwa na
lengo la kutengeneza katiba ya chuo hicho.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment