MAHAKAMA NCHINI TANZANIA YAWAACHIA HURU WAANDISHI WA HABARI!!


Absalom Kibanda akizungumza na waandishi.
                                            Absalom Kibanda akizungumza na waandishi.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru  Meneja Uendelezaji Biashara wa Mwananchi Communications (MCL), Theophil Makunga, aliyekuwa Mhariri Mtendaji  wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.
Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika(VOA ) Absalom Kibanda ambaye pia ni  Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri amesema maamuzi ya mahakama hiyo yamerejesha  matumaini mapya kwa tasnia ya habari kwa wanahabari na vyombo vya habari kwamba pamoja na sheria kandamizi wanayo  fursa ya kushinda  baadhi ya hila, baadhi ya mipango ya kudhulumu vyombo vya habari  nchini  Tanzania.

Akielezea maamuzi ya mahakama hiyo amesema kwamba mahakama iliamua kuwa  serikali ilifungua kesi hiyo katika misingi ya hisia kwani yalioandikwa ni masuala ya kawaida hakukuwa na nia ya uovu, waandishi walitumia uhuru wao wa kujieleza  na hakukuwa na matukio yeyote ya wazi kwamba baada ya ile makala kumekuwa na vitendo au matukio yaliotokana na uandishi wa makala hiyo.
Amesema maamuzi hayo yatalazimisha mabadiliko kwani ni sawa na kujifunza kwa viboko kwani kuna dhamira mbaya na chuki za wazi dhidi ya vyombo vya habari, ni fundisho  kwamba lazima walio madarakani, waandishi   na wananchi wa kawaida wanapaswa kujifunza  kwamba  hakuna aliye juu ya sheria.

 Amesema wana imani kupitia mchakato wa katiba mpya kuwa wataweza kupata fursa ya kuingiza masuala mengi yanayohusu uhuru wa vyombo vya habari katiba katiba mpya ijayo nchini humo.

Akielezea zaidi kuhusu chuki dhidi yao amesema upande mmoja ni kwasababu ya waandishi wenyewe na kwa upande mwingine viongozi walioko madarakani hawapendi kukosolewa kutokana na tabia zao akitolea mfano  matumizi mabaya ya madaraka ya Polisi. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment