Mnara wa Mwenge uliopo katikati ya Jiji la Arusha |
kukamata wauzaji wa nguo za ndani za mitumba ambazo zimepigwa marufuku
katika maeneo mbalimbali hapa nchini, zoezi ambalo ni mwendelezo kwa
nchi nzima.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo,Afisa viwango wa shirika hilo Bw. Paul Manyilika alisema kuwa, oparesheni hiyo ilianzia jijini Dar es Saalamu ambapo zoezi hilo ni endelevu na litafanyika katika mikoa yote nchi nzima na katika zoezi hilo wafanyabiashara sita wamekamatwa
na nguo zao baada ya kukutwa wakifanya biashara hiyo katika eneo la soko la Kibokoni lililopo mjini hapa . .
Alisema kuwa,Shirika hilo linahitaji kudhibiti uingizwaji wa nguo za ndani za mitumba ambazo zina madhara makubwa kwa watumiaji kutokana na kutojulikana kiwango cha kemikali kilichotumika katika utengenezaji wa nguo hizo.
Aidha alisema kuwa, eparesheni hiyo wamekuwa wakiifanya kwa kushirikiana na jeshi la polisi ,ambapo wamekwisha ziba maeneo yote ambapo nguo hizo zinaiingilia , hivyo wanawataka wafanyabiashara wanaoendelea kuuza nguo hizo ili waweze kueleza wanapozipata.
"zoezi hili tangu limeanza limefanikiwa kwa kiasi kikubwa ,kwani wahusika wameweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria , ikiwa ni pamoja na kuteketeza nguo hizo kwani hazitakiwi kuonekana kabisa hapa nchini."alisema Manyilika.
Alisema kuwa,matumizi ya nguo za ndani yana madhara makubwa kwa watumiaji kwani zinakuwa zimeshavaliwa na wengine, wakati kuna viwanda vikubwa hapa nchini vinavyoweza kutengeneza nguo hizo kwa usalama
zaidi na bila kuwa na madhara yoyote.
Aidha alitoa wito kwa wafanyabiashara wanaoendelea kuuza nguo hizo kuacha mara moja kwani nguo hizo zimepigwa marufuku ,kutoka na kuleta madhara mbalimbali kwa watumiaji wake .
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa shirika hilo, Bw.Baptister Bitaho alisema kuwa, zoezi hilo ni halali kabisa na wafanyabiashara wanaofanya biashara hizo, walishapewa notisi ya kusitisha uuzaji wa nguo hizo masokoni , ila wengine bado wanaendelea hivyo zoezi hilo bado linaendelea na litafanyika nchi nzima.
Bitaho alisema kuwa, endapo mtu atabainika kuhusika na uuzaji wa nguo hizo ambazo zimepigwa marufuku ,adhabu yake ni shs 50 milioni hadi shs 100 milioni au kifungo cha miaka miwili jela .
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment