WAKATI David Moyes akikongwa moyo na
mwanzo mwema wa Mchezaji mpya Juan Mata na kurejea Uwanjani kwa Robin
van Persie na Wayne Rooney kulikowapa ushindi Jana, Arsene Wenger
amesononeshwa na kudhoofika kwa Kiungo cha Timu yake baada Jana
kumpoteza Mathieu Flamini kwa Kadi Nyekundu na pia kuendelea kuwa nje kwa maumivu kwa Aaron Ramsey.
MOYES NA MATA, VAN PERSIE NA ROONEY
Meneja wa Manchester United, David
Moyes, amesema kumsaini Juan Mata na kurejea Uwanjani kwa Robin van
Persie na Watne Rooney kutoka kwenye maumivu ambako Jana kuliwapa
ushindi walipoichapa Cardiff City Bao 2-0 Uwanjani Old Trafford kumeleta
hali mpya kwenye Timu yao.
Van Persie Jana alirejea Uwanjani baada
kuzikosa Mechi 11 na Juan Mata alicheza Mechi yake ya kwanza tangu
ahamie kutoka Chelsea hivi Juzi huku Rooney akianzia toka Benchi katika
Mechi yake ya kwanza tangu Januari Mosi.
Mwenyewe Mata alibainisha kufurahishwa
na mapokezi yake Man United na pia kuridhika na uchezaji wake kwenye
Mechi yake ya kwanza ingawa alikiri anahitaji kufanya Mazoezi zaidi
baada ya kuyakosa Wiki iliyopita kwa ajili ya hekaheka za Uhamisho.
Nae Moyes amekiri kuwepo kwa Mastaa hao watatu kumeleta matumaini mapya ingawa alisema bado ipo kazi kubwa.
Akimwongelea Mata, Moyes alisema: “Juan
alifanya vyema. Alitengeneza nafasi zetu bora katika Dakika 30 za
kwanza. Tutamzoea na atatuzoea. Nilitaka kuwaona yeye na Robin wakicheza
pamoja. Tutamtumia katika nafasi kadhaa tofauti.”
Kuhusu Mata, Rooney na Van Persie kucheza pamoja, Moyes alisema: “Wakiwemo kwenye Timu, matokeo yatazidi kuwa bora!”
WENGER ASONONEKA KUDHOOFIKA KIUNGO!!
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesononeshwa na kudhoofika kwa Kiungo cha Timu yake baada Jana kumpoteza Mathieu Flamini kwa Kadi Nyekundu na pia kuendelea kuwa nje kwa maumivu kwa Aaron Ramsey.
Jana Kiungo wao Mathieu Flamini alipewa
Kadi Nyekundu walipotoka Sare ya Bao 2-2 na Southampton na hiyo
inamaanisha atazikosa Mechi zijazo za Arsenal dhidi ya Crystal Palace,
Liverpool na Man United.
Sare hiyo imewakosesha Arsenal kuzidi
kupanda kileleni na kuwa Pointi 4 juu na hii inaweza kuwafanya
waporomoke hadi Nafasi ya 3 ikiwa leo hii Man City na Chelsea zitashinda
Mechi zao.
Man City wanacheza na Tottenham huko
White Hart Lane na Chelsea wako kwao Stamford Bridge kuikabili West Ham
na wakipata ushindi wa tofaut ya Bao 2 wataipiku Arsenal.
Pia Wenger alitoboa kuhusu kuendelea kuumwa kwa Aaron Ramsey ambae hajapona matatizo ya Paja lake.
Wenger amekiri kuwakosa Flamini na Ramsey kumedhoofisha sana sehemu ya Kiungo ya Timu yake.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA YA LEO:
[Saa za Bongo]
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
23 |
24 |
52 |
2 |
Man City |
22 |
38 |
50 |
3 |
Chelsea |
22 |
23 |
49 |
4 |
Liverpool |
23 |
29 |
46 |
5 |
Tottenham |
22 |
3 |
43 |
6 |
Everton |
23 |
11 |
42 |
7 |
Man Utd |
23 |
11 |
40 |
8 |
Newcastle |
23 |
4 |
37 |
9 |
Spton |
23 |
4 |
32 |
10 |
Swansea |
23 |
-4 |
24 |
11 |
Aston Villa |
22 |
-7 |
24 |
12 |
Norwich |
23 |
-17 |
24 |
13 |
Hull |
23 |
-7 |
23 |
14 |
Crystal |
23 |
-16 |
23 |
15 |
West Brom |
22 |
-5 |
22 |
16 |
Stoke |
22 |
-14 |
22 |
17 |
Fulham |
23 |
-28 |
19 |
18 |
West Ham |
22 |
-11 |
18 |
19 |
Sunderland |
22 |
-15 |
18 |
20 |
Cardiff |
23 |
-23 |
18 |
0 comments:
Post a Comment