Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo |
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na
kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani
uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23.
Akitoa
shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema
leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia
wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba
hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na
utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya
kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na
vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia
gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapendi vurugu, wamezoea
amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi
kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.
Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni
(Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na
Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo,
Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa
(Morogoro) na Mrijo (Dodoma).
0 comments:
Post a Comment