FULHAM MAJI SHINGONI,NAYE LAUDRUP APIGWA BUTI!!


SWANSEA CITY imemtimua kazi Meneja wao Michael Laudrup na kumweka Nahodha wao Garry Monk kama Meneja wa muda.MICHAEL_LAUDRUP
Laudrup, ambae ni Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Denmark aliewahi kuzifundisha Klabu za Brondby, Getafe, Spartak Moscow na Real Mallorca, ametimuliwa baada ya Jumamosi kufungwa 2-0 na West Ham kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.


JE WAJUA?
-Laudrup ni Mchezaji pekee aliewahi kutwaa Ubingwa wa Spain mara 5 mfululizo akiwa na Klabu mbili tofauti, Real Madrid na Barcelona.
-Laudrup pia alitwaa Ubingwa akiwa Mchezaji wa Juventus na Ajax.

Hicho kilikuwa kipigo chao cha 6 katika Mechi 8 za Ligi zilizopita na kimewaacha wapo Pointi 2 tu juu ya zile Timu 3 za mwisho mkiani.
Laudrup aliteuliwa Meneja wa Swansea Juni 2012 kumrithi Brendan Rodgers alieenda Liverpool na aliweza kuifanya Swansea itwae Kombe la Ligi Mwaka Jana na Msimu huu kucheza UEFA EUROPA LIGI na wapo Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ambapo baadae Mwezi huu watacheza na Napoli ya Italy.
FA CUP-Marudio Raundi ya 4: Fulham 0 Sheffield United 1
Bao la Dakika ya 120 la Shaun Miller, alietoka Benchi limewapa ushindi Sheffield United wa Bao 1-0 katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya 4 ya FA CUP iliyochezwa Craven Cottage Jana Usiku na kuwa Sare 0-0 hadi Dakika 90 zinaisha.
Sheffield United, ambayo iko Madaraja mawili chini ya Fulham, kabla ya Mechi hii ilikuwa haijashinda katika Mechi zao 5 za Ugenini.
Kipigo hiki ni mwendelezo mbovu kwa Fulham ambao kwenye Ligi Kuu England wako Nafasi ya mwisho.
Kwenye Raundi ya Tano ya FA CUP, Sheffield United watacheza na Mshindi kati ya Preston North End na Nottingham Forest.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment