Programu hiyo itawahusisha wenyeviti wote wa serikali za mitaa pamoja
na askari, yenye lengo la kuboresha masuala ya usalama katika Jiji la
Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa ufunguzi wa
programu hiyo ambayo imeanza katika Mkoa wa Ilala, Kamishna wa Polisi,
Suleiman Kova, alisema wameamua kufanya hivyo wakiamini kwamba katika
kila mtaa watu wanaofanya uhalifu wanajuana.
Alisema serikali za mtaa watashirikiana na polisi kushughulikia vitendo vya uhalifu kwani wapo karibu na wananchi.
“Tunaamini kwamba bila ushirikiano kati ya viongozi mbalimbali na
polisi ulinzi hauwezi kuimarika, hivyo kwa kufanya hivi imani yangu
uhalifu utaisha kabisa kwani kila mtaa utajitegemea katika ulinzi wake
chini ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa,” alisema.
Hata hivyo, Kova alisema wataandaa tuzo na kushindanisha mtaa kwa
mtaa ambapo ule utakaokuwa umefanikiwa kudhibiti uhalifu kwa kiasi
kikubwa utapata zawadi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gerezani, Ramadhani Matibwa,
alisema wakiwa kama viongozi wanawajua wahalifu hivyo kwa mpango huo
utasaidia kupunguza wahalifu na kuwarahisishia kazi Polisi.
“Tumefurahi sana kwani uhalifu ulikuwa umekithiri sana, kwa kuwa kila
mtaa utajitegemea katika ulinzi wake utarahisisha upatikanaji wa
taarifa kuliko zamani ilikuwa mpaka upige simu polisi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment