Serikali imesema haina Ugomvi na vyombo vya habari hapa nchini kama ambavyo baadhi ya vyombo hivyo vimekuwa vikiripoti.
Akizungumza
leo katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa
Serikali Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella
Mukangara alisema haoni sababu ya kuingia kwenye ugomvi na wadau muhimu
kama vyombo vya habari.
“Kuna
wanaozunguka zunguka wakieleza kwamba kuna ugomvi kati yetu na vombo
vya habari, mkiwasikia wapuuzeni”.alisema waziri Mukangara.
Dkt
Mukangara alipongeza kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya habari na
kuvitaja kuwa wadau muhimu wa Serikali katika kuwaletea wananchi
maendeleo na kutoa taarifa.
Dkt.Mukangara
aliongeza kuwa ni jukumu la Maafisa Habari na Mawasiliano kuwaunganisha
wananchi na Serikali kwa kutoa taarifa zitakazowasaidia wananchi
kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akifafanua
zaidi Dkt. Mukangara amesema kuwa Wizara itaendelea kuratibu mikutano
ya Taasisi za Serikali na Vyombo vya Habari ili kuwapa wananchi fursa ya
kujua mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali.
Katika
Utaratibu huo Dk Mukangara amesema mikutano 156 kati ya taasisi za
Serikali na Vyombo vya Habari ilifanyika kati ya 204 iliyotarajiwa
kufanyika katika kipindi cha julai hadi Desemba 2013 ikiwa ni
utekelezaji wa jukumu la msingi la kuwapa wananchi taarifa kwa wakati.
Pia
aliwaasa Maafisa Habari na Mawasiliano kote nchini kujituma na kufanya
kazi kwa weledi ili kuwasaidia Taifa kufikia maendeleo endelevu.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel Alibainisha
kuwa Mafunzo kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii katika kuimarisha
mawasiliano ya Serikali kwa umma.,mafunzo ya vitendo kuhusu matumizi ya
mitandao ya kijamii na mada kuhusu namna bora ya kutumia na kuendesha
radio za kijamii.
Kauli
mbiu ya Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano zaidi ya 100 toka
Tanzania nzima ni Matumizi ya Tehama na Mitandao ya Kijamii katika
kuimarisha Mawasiliano ya Serikali kwa umma.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment