WAFUGAJI WASHAURIWA KUFUGA KISASA!!

MBUNGE wa Longido Lekule Laizer (CCM), amewashauri wafugaji nchini kuachana na ufugaji wa kienyeji na kuanza kufuga kisasa ili kuongeza thamani ya mazao ya mifugo yao.

Ushauri huo ameutoa hivi karibuni wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho ili kuwashukuru baadhi ya wabunge waliofanikisha kukomesha operesheni mbalimbali zilizokuwa zikiua mifugo yao.
Alisema kuwa wafugaji wengi nchini wamekuwa wakifuga mifugo isiyokuwa na tija kwa kufuga ng'ombe ambao mbegu zao ni ndogo hivyo kupata fedha kidogo kutokana na ufugaji wa aina hiyo hivyo kuwashauri kuachana na ufugaji huo na kuanza kufuga kisasa kwa kutafuta mbegu nzuri za madume ya ng'ombe ambayo zinakuwa kwa haraka na pindi zinapopelekwa sokoni huweza kuuzwa kati ya sh. milioni 1.5 hadi milioni 2.
Aidha aliwataka wafugaji hao kuheshimu maeneo ya wakulima ili kuepusha migogoro ambayo kwa siku za hivi karibuni imesababisha ugomvi na mauaji na kusema kuwa hata kama Serikali itatenga maeneo ya wafugaji kama hawataheshimiana na kujua mipaka yao ni lazima migogoro hiyo itaendelea na kuzidi kuhatarisha amani ya wafugaji nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wafugaji kutoka kanda ya Ziwa Venance Kabwebwe aliwalaumu watendaji wakuu wa Serikali wenye dhamana na wafugaji kuwa ndiyo chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuwa hawana msaada wowote katika kukabiliana na migogoro hiyo pindi wanapopata taarifa kwa kushindwa kuitatua kwa haraka.

Chanzo;Mwananchi

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment