Wakati mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na
kufanyiwa dua kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini
na wakati huo huo unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya
kutumikia ofisi kubwa na ya Heshima kuliko zote Nchini , nimekuwa
nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko Nyuma mwaka
jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla
mambo hayajaaribika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa
ambao siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma na Nape na wenzake pia
walipata fursa ya kuusoma .
Mh Rais katika waraka hule nilisema hivi “
Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile nilichosema
katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea
katika Taifa lako na langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo
kidogo sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi mwako kwani hali ya
Nchi sio nzuri hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na
upendo sasa wanaanza kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.
Mh Rais,
Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama vya
upinzani na yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na
mkakati huo unaendelea dhidi ya Chadema lakini kinachosikitisha ni kuwa
wale waliobuni mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara yake
mbele .
Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na
Ukanda hauishi tu kuangamiza hicho Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa
Ujumla , Mtu anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha Wakristo kimsingi
matamshi hayo hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya
Udini wao na na kufanya Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na
hivyo mpango huo unafanya Watu waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila
na matokeo yake ndiyo haya tunaanza kuyaona leo .
Mh Rais, Taifa
linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita kwenye mgogoro
wa Waisilamu na Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye vyombo
vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa busara zile zilizokuwa zimejaa
hofu kubwa .
Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu
anayepaswa kuchinja?Mh Rais , Nilipoona jambo hili nilianza kujiuliza
maswali mengi sana, kwanza , umakini huu kwa pande zote mbili juu ya
jambo hili umeletwa na nini na nani? Kwani yako mambo mengi
yaliyokatazwa na Biblia na Msaafu ambayo watu wote wa dini hizi mbili
wamekataa kuyatii au kuyafuata , kwa mfano waislamu na wakristo vijana
kwa wazee wanakunywa pombe pamoja baadhi yao kujenga mahusiano hata ya
kimapenzi yasiyo rasmi bila hata kufuata utaratibu wa Msaafu wala Biblia
lakini hapa hutaona ugomvi mkubwa sana japokuwa ni masuala yanayo mkera
na kumuudhi mwenyezi Mungu sana.Mh Rais , ndio maana katika suala hili
la nani achinje kati ya Muislamu na Mkristo niliposikia maafa yake
nikakumbuka waraka niliokuandikia mwaka jana kuhusu choko choko za Udini
ambazo zimeanza kuleta maafa ambazo Mwanzilishi wake ni CCM.
Mh Rais
Chama chako unachokiongoza , Team yako imekuwa ikifanya sana propaganda
hizi za, Udini , Ukabila , na Ukanda usiku na mchana , lakini nimekuwa
nikikerwa sana na Jinsi kabila la Wachaga linavyochukuliwa katika
propaganda hizi na wanaofanya hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa
Wachaga na mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na
Ukabila wakati wao wenyewe ni familia moja ?Kwa mfano , Mh Mwigulu
Nchemba , Mh David Mathayo , Mh January Makamba , Mh Benjamin Mkapa , Mh
Fredrik Sumaye , Mh Theo , Mh Dr Faustin Ndungulile , Mh Prof Ibrahimu
Lipumba , Pro Mahalu , Mh Dr Hamis Kigwangala , Mh John Mgufuli , Mh
Sospeter Muhongo , Mh Jaji Warioba, Idd Simba, Mh Salmin Amour , na
wengine wengi wote hawa wameoa Kilimanjaro .
Sasa unajiuliza hawa wote
ni Viongozi ndani ya CCM na wengine ndio mabingwa wa kufanya Siasa za
Udini na Ukanda , je wake zao ndani ya nyumba wanajisikiaje wanapoona
waume zao wanatukana kabila za ndugu zao kwa sababu ya Siasa ?
Hii ni
hatari kubwa Mh Rais kama kuchinja ni suala zito kiasi hicho katika
Imani ya Kiislamu na pia ni neno kutoka katika Kitabu cha Imani yao basi
ni haki na kweli kuwa wao wanapaswa kuchinja kwa Imani ya Dini yao na
wala wasilazimishwe kumkosea Mungu wao kwani hakuna maarifa na Busara
inayozidi imani, lakini vile vile Wakristo wasilazimishwe kushiriki
Ibada ambayo sio yao. Waislamu kama wanaamini kuwa wao kuchinja ndio
jambo lililoamrishwa katika vitabu vyao basi sasa Jambo hilo liheshimiwe
na kutafutiwa utaratibu na vile vile Wakristo wasipuuzwe kugoma
kushiriki jambo ambalo kwa wengine lina sura ya Imani.Nini
Kifanyike?
Kwanza Chama chako na Viongozi wake uwakanye na kuwashauri
mara moja kabisa kuacha propaganda za udini na ukanda , kwani katika
hili hakuna namna Nchi inaweza kubaki salama , kwani hizo choko choko
hazitokani na nia mbaya ya Waislamu na Wakristo bali ni siasa chafu
iliyopandikizwa ili kuangamiza vyama vya Siasa na sasa imekwenda zaidi
na imeanza kuwatesa wakati ambao Nchi ina matatizo mengi ,
Kwa mfano
Chadema tulipoandama Arusha kupinga Uchaguzi wa Meya feki , Kiongozi
mmoja wa Mkoa wa CCM hapa Arusha , alinukuliwa na vyombo vya habari
akidai tunafanya maandamano hayo kwa sababu za Udini na ndio maana
hatumtaki Meya , lakini kitu cha kushangaza huyu Meya Feki ni Mkristo
tena Mchaga Kabila langu , lakini niliambiwa na tunampinga na Maaskofu
wanampinga kwa sababu Chadema ni Chama cha Udini ‘ sasa najiuliza kama
Meya huyu Feki ni Mchaga na ni Mkristo je hayo madai ya kijinga yanatoka
wapi ?
Kama Ukristo ni ajenda kubwa kwetu kwani nini tulimpinga sasa ?
Huu ni mfano mmoja iko mingi sana inayoashiria mkakati wa makusudi wa
kuangamiza Chadema na huku mkisahau kuwa maliangamiza Taifa , na ndio
Mkuu wa Mkoa wa Arusha alipokuja tu alidai kuwa amekuja kupambana na
Chadema na Wachaga , ila nimuhakikishie hataweza na asijaribu kamwe na
mikutano ambayo amekuwa akiifanya aiche mara moja .
Pili, Mh Rais,
ninaamini kuwa wewe umesafiri Nchi mbali mbali kuliko mimi , Ukienda
Marekani , Spain , Brazil , China , Hong Kong , UK, Italy , Sweden,
Botswana , Namibia , South Afrika , Zimbabwe na Nchi nyiongi utaona
Maduka au Mabucha ya Nyama yameandikwa (Halal ) au unanua bidhaa yeyote
ya aina ya Nyama na kukuta imeandikwa “Halal” na ni ustarabu kwamba
bidhaa hiyo machinjio yake yamezingatia maadili ya Dini ya Kiislamu na
Waislamu wenye Imani thabiti na Imani yao hapo ndipo watakapofanya
manunuzi yao katika bidhaa hiyo ya aina ya Nyama.
Lakini maeneno hayo
hayo unaweza kupata nyama katika maduka mbali mbali yasiozingatia
utaratibu huo na kwa hivyo watu wasiojali sana masuala ya Imani wala
hawatasumbuka kuuliza na kusoma kama Nyama hiyo imezingatia masuala ya
matakwa ya Imani Fulani.Hivyo, Mh Rais, nafikiri ni vyema utaratibu huu
ukaletwa hapa kwetu ili tuonyeshe Kujali Imani ya Waislamu katika Jambo
hili ambalo limekuwa kwazo katika Jamii hizi mbili kubwa na kama
ufumbuzi wake hautakuwa kuzingatia hili basi tarajia uchungu kuendelea
kutembea kwenye vifua vya watu bila kusema na siku moja hali inaweza
kuwa mbaya na tukapoteza Taifa.
Mh Rais, naiona hofu isiyokuwa ya kweli
ya Mh Waziri Mkuu kuwa tukiruhusu hilo kuwa Wakristo na Waislamu
wataweza kutengana kwenye mambo mengine mengi haswa katika Biashara na
mambo mengine , kitu ambacho nasema sio kweli kwani , Sukari ,Mchele ,
Soda na Juisi na bidhaa nyingi hazina makatazo na maelekezo katika Imani
, Mfano kila Mkristo anajua kuwa Mwislamu hatumi Nguruwe na Nguruwe kwa
mwislamu ni haramu na hivyo Mkristo hawezi kupika Nguruwe na huku
akijua kuwa wageni wake siku hiyo ni Waislamu.Kwa hiyo hofu ya kuligawa
Taifa kwa kurusu jambo hili haliwezi kutokea kwani ni miiko ya Kiimani
ambayo pande zote zinapaswa kuheshimiana ili upande mmoja usione
umekandamizwa na kupuuzwa , na hofu ya kibiashara inayoweza kutokea
katika suala hili inapaswa kupuuzwa kwani IMANI ni zaidi ya Biashara
japokuwa sioni jambo hili likitokea .
Mh Rais, nisikuchoshe sana, lakini
haya ni maoni yangu na Mke wangu na sio Chama changu tumeamka leo
Asubuhi tukasema tukuandikie tena kwani wewe ni Mkuu wa Nchi , Najua
unaweza kuwa busy sana kusoma waraka huu mrefu ila najua Mwigulu na Nape
lazima wausome na Rizwan pia hivyo niwaombe wakufikishe ujumbe huu kwa
niaba ya familia yangu.Mh Rais , We are pressed on every side by
troubles, but not crushed and broken. We are perplexed because we don,t
know why things happen as they do .
But we don’t give up and quit, we
are hunted down BUT God never abandons Us, We get knocked down BUT we
get up again and keep going. The root of life need commitment and
there’s a lot of suffer to get at the Climax. Don’t Give Up Mr President
please, Help our Country now.Godbless Jonathan Lema
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment