Mkufunzi wa Masuala ya Kijinsia Bi. Tumaini Kyola akitoa mafunzo kwa kundi la Wasichana 30 ambao hawako mashuleni juu ya mbinu mbalimbali za kuelemisha jamii kuhusu masuala Ukatili wa Majumbani na w http://victorndanshau.blogspot.comkingono pia. Wasichana hawa wanategemewa kwenda kuwafundisha wasichana wenzao wa mitaani, kila mmoja amepewa lengo la kufikia wasichana 50. |
Mkurugenzi
wa shirika la kutetea Haki za Wanawake na Wasichana KIVULINI lenye
makao yake makuu jijini Mwanza Bw. Ramadhan Masele amefunga rasmi
mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea wasichana uwezo wa kutoa
elimu juu ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia chini ya
mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili wa majumbani ikiwa ni
pamoja na ukatili wa kingono kwa watoto wa kike na wasichana.
Akizungumza
na washiriki wa mafunzo hayo Bw. Masele aliwataka washiriki wote
kutumia elimu hiyo muhimu waliyoipata kutoa elimu na kuongeza uwelewa
zaidi kwa jamii yao kuanzia ngazi ya familia, marafiki na vikundi
mbalimbali na kuwa chachu ya mabadiliko juu ya kupigania haki za
wanawake na wasichana wanaonyanyaswa kijinsia katika jamii zao.
“Imani
yangu ni kuwa semina hii itakuwa ni kiwanda kizuri cha kuwatengeneza
nyinyi wote kuwa mabalozi wazuri katika jamii, baada ya mafunzo haya
tunaamini kuwa mtakuwa chachu ya mabadiliko katika kutetea na kulinda
haki za wanawake na wasichana kwa kukemea, Kupinga, kuripoti na kuzuia
aina zote za ukatili wa majumbani na kingono kwa wasichana na wanawake
na kutoa taarifa pindi vitendo hivi vinapotokea” alisema Bw. Masele
“Kila
mmoja aliyehudhuria mafunzo haya kwa nafasi aliyonayo tunaamini
anaweza kuwa chachu ya mabadiliko endapo atatimiza wajibu wake kwenye
eneo analoishi. Hili suala la ukatili wa kijinsia si suala geni nchini
hasa eneo hili la kanda ya ziwa hivyo kuna kila sababu ya kuzidisha
mapambano dhidi yake, cha muhimu ni kuzingatia mafunzo mliyopewa na
muwezeshaji wenu” aliongeza Bw. Masele.
Mafunzo
hayo yamefanyika kwa muda wa siku 5 kwa vijana 30 wa kike wenye umri
kati ya miaka 18-24 kutoka wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini
Mwanza. Lengo la Mafunzo ni kuwajengea vijana uwezo wao binafsi na uwezo
wa kuelimisha jamii hasa Vijana wenzao kupambana na kupinga Ukatili
dhidi ya wanawake na wasichana katika maeneo wanayoishi.
Mafunzo
yalianza Jumatatu tarehe 28 Aprili, 2014 mpaka tarehe 2 Aprili, 2014
katika Ukumbi wa Chuo cha Ufundi Stadi, VETA kilichopo Nyakato nje
kidogo ya jiji la Mwanza.
Takwimu
zinaonyesha bado jamii inakabiliwa na ukatili mkubwa wa kijinsia ambapo
ubeberu wa wanaume pamoja na mila na desturi potofu zimeonekana
kukandamiza jinsi ya kike zaidi kuliko jinsi ya kiume, ukatili huo ni wa
kijamii, kiuchumi pamoja na kisaikolojia hivyo kunaitajika juhudi za
dhati na makusudi kuweza kukabiliana na tatizo lilopo kwa jamii.
Akimalizia
mawaidha yake kwa washiriki Bw. Masele alisema lengo la mafunzo hayo ni
kuona mabadiliko katika mfumo juu ya kujali na kuheshimu haki za
mwanamke na wasichana, kwani jamii nyingi zinapambana na mifumo miwili
mikubwa, ambayo ni mfumo dume ambao umekuwa ukiwakandamiza wanawake
katika jamii na mfumo wa kitabaka unaoongeza nafasi kati ya matajiri na
masikini.
Shirika
la KIVULINI kwa kushirikiana na Asasi ya Vijana inayojulikana kama
Wadada Centre for Solution Focus Approach ndio waandaji wa mafunzo hayo
kupitia mradi wa kuwashirikisha vijana kuzui Ukatili majumbani na
Ukatili wa Kingono chini ya ufadhili wa Shirika la terre des hommes ch
(tdhschweiz) - Fursa kwa Vijana la nchini Switzerland
0 comments:
Post a Comment