Home / Uncategories / KAMATI YA MWENYEKITI WA BUNGE MAALIMU LA KATIBA SAMUEL SITTA YAIUNDIA UKAWA ZENGWE!!
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta akisisitiza
jambo jana, baada ya mkutano wa Kamati ya Maridhiano uliofanyika jijini Dar es
Salaam.
Taarifa hizo zilieleza kuwa kama akidi haitatimia moja ya
mambo yatakayofanywa ni pamoja na Watanzania kuelezwa jinsi kususa kwa Ukawa
kunavyokwamisha mchakato huo.
Sitta aliitisha kikao hicho cha wajumbe 30 wakiwamo viongozi
wa Ukawa jana, akisema kilikuwa na lengo la kutathmini mwenendo wa vikao vya
Bunge Maalumu la Katiba na kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuondokana na
mgawanyiko uliopo.
Licha ya mwaliko huo, hakuna mjumbe yeyote wa Ukawa
aliyehudhuria, lakini kwa upande wa vyama vya upinzani wajumbe waliohudhuria ni
Peter Mziray wa APPT-Maendeleo na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed
ambaye alisimamishwa uanachama wa chama hicho.
“Uamuzi wao (Ukawa) unaweza kukwamisha mambo mengi ikiwa ni
pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2015. Ila kifupi vikao
vitaendelea na lolote linaweza kutokea. Uamuzi utategemea na akidi
itakayokuwapo,” kilisema chanzo chetu ndani ya mkutano huo.
Hata hivyo, mjumbe mwingine wa kikao hicho cha jana alisema:
“Unajua katika kikao imeonekana wazi kuwa akidi itatimia kwa kuwa theluthi
mbili ya wajumbe kutoka Zanzibar itatimia tu.”
Habari kutoka katika kikao hicho cha siku mbili kilichoanza
jana saa nne asubuhi na kumalizika saa 8:14 mchana, zilieleza kuwa mvutano
mkali uliibuka kuhusu akidi ya wajumbe kwa ajili ya kupitisha uamuzi katika
Bunge hilo.
Kifungu cha 26 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinaeleza:
“Ili Katiba inayopendekezwa iweze kupitishwa katika Bunge Maalumu, itahitaji
kuungwa mkono kwa wingi wa theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa Bunge
Maalumu kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote wa
Bunge Maalumu kutoka Tanzania Zanzibar.”
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili Julai 8, mwaka huu,
Sitta alisema iwapo Ukawa watarudi bungeni lakini wakasusa tena kadri mjadala
utakavyoendelea, Bunge litaangalia upya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo
inataka theluthi mbili kufanya uamuzi.
Hata hivyo, wazo hilo tayari limepingwa na wanasheria
mbalimbali wakisema suala hilo haliwezekani kwa kuwa Bunge la Muungano lenye
dhamana ya kutunga sheria halitakuwa na kikao hadi Novemba na kwamba hitaji la
mambo ya Muungano kuamuliwa kwa theluthi mbili ya wajumbe kutoka kila upande si
tu la kisheria, bali pia ni la kikatiba.
Vilevile, mwenyekiti huyo alidokeza kuwa mkutano wa jana
ungekuwa kipimo cha kuwaonyesha Watanzania iwapo Ukawa wako tayari kwa Katiba
Mpya au la.
Taarifa zaidi zilifafanua kuwa hoja ya Ukawa ya kutaka
ijadiliwe Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nayo
iliibuliwa katika kikao hicho jana, lakini ilipingwa kwa maelezo kuwa Rasimu
hiyo inaweza kubadilishwa na si kuboreshwa pekee.
Awali, jana Sitta alisema kuwa atatoa ufafanuzi wa
kilichojadiliwa katika kikao hicho saa 10 jioni, lakini baadaye alituma ujumbe
kwamba atafanya hivyo leo saa tatu asubuhi na baadaye muda huo ukaongezwa kuwa
itakuwa saa tano asubuhi.
Alipoulizwa kama akidi isipotimia nini kitafanyika, Sitta
alisita kujibu swali hilo na kueleza kuwa atakapotoa ufafanuzi kwa wanahabari
atafafanua jambo hilo.
Kwa nyakati tofauti, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda wamenukuliwa wakisema kuwa iwapo Katiba Mpya haitapatikana
itaendelea kutumika ya sasa ingawa italazimika kufanyiwa marekebisho katika
maeneo fulani, ambayo hawakuyataja baada ya maridhiano na pande zote.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment