Kauli hiyo ya Rais Kikwete aliitoa jana
alipokutana na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu
wa China,
Kauli hiyo inapingana na ile ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania (AG), Jaji Frederick Werema ya hivi karibuni kwamba kura hiyo ingefanyika Machi 30, mwakani.
Kauli hiyo inapingana na ile ya Mwanasheria Mkuu wa Tanzania (AG), Jaji Frederick Werema ya hivi karibuni kwamba kura hiyo ingefanyika Machi 30, mwakani.
Mbali na Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva alisema juzi mjini Dodoma kwamba
kura ya maoni haiwezi kufanyika Machi 30 mwakani kwa sababu kazi ya
uandikishaji wa daftari la wapigakura haitakuwa imekamilika.
Rais Kikwete aliwaambia mabalozi hao kuwa mchakato
wa Tanzania kusaka Katiba Mpya unakwenda vizuri baada ya kupitia hatua
zote ikiwamo ile ya kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kuundwa
kwa Tume ya Kukusanya Maoni ya Wananchi na Bunge Maalumu ya Katiba
ambalo lilipigia kura ya kuipitisha Katiba Inayopendekezwa.
“Lililobakia sasa ni Kura ya Maoni ya Wananchi.
Tunadhani kuwa kama itakwenda kama tulivyopanga, kura hiyo itapigwa
wakati wowote Aprili mwakani. Bado tunaangalia tarehe mwafaka kwa ajili
ya shughuli hiyo muhimu,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katiba hiyo ikipita, sote tutashangilia na
kusherehekea lakini matokeo ya Kura ya Wananchi yakiwa tofauti, basi
tutaendelea kuongozwa na Katiba ya sasa mpaka huko mbele wakati nchi
yetu na wananchi watakapoamua tena kujaribu kupata Katiba Mpya.”
Jaji Lubuva
Akizungumza katika semina ya Baraza la Vyama vya
Siasa mjini Dodoma, Jaji Lubuva alisema itakuwa vigumu kufanyika kwa
kura hiyo Machi 30 kama ilivyotangazwa na Jaji Werema kwani kazi ya
uandikishaji wa daftari la wapigakura imechelewa kuanza kutokana na
sababu mbalimbali ikiwamo kukosekana fedha.
“Serikali imeshatuhakikishia itafanya malipo na
kati ya sasa na Desemba baadhi ya vifaa vinaanza kuja. Malipo
yakishafanywa katika miezi hiyo mitatu; Januari, Februari na Machi
tutajitahidi kila iwezekanavyo kuboresha daftari.”
Jaji Lubuva naye alisisitiza kuwa Tume yake haitafanya uchaguzi au kura ya maoni kama daftari halijaboreshwa.
“Naona kuna gazeti moja (Mwananchi) lilisema Kura
ya Maoni ni Machi 30 mwakani, haiwezekani. Tulisema Januari, Februari,
Machi sasa unaposema Machi 30, mwezi Machi haujaisha kwa hiyo ni tarehe
ambayo itakuja baada ya hapo,” alisema.
Alisema ikiwa mambo ya fedha yatakwenda kama
alivyosema AG, Tume itajitahidi kwa kipindi hicho cha miezi mitatu
kukamilisha kazi hiyo.
Utata mwingine
Wakati mvutano wa tarehe ya kura hiyo ukiendelea,
imebainika kuwa wakati Hazina ikihangaika kulipa Sh149 bilioni za Mfumo
wa Utambuzi wa Mpigakura wa Kielektroniki (BVR), Ofisi ya Waziri Mkuu
imekataa ofa kutoka Ufaransa na Canada ya kutoa mashine 12,233 kupitia
ushirikiano wa serikali kwa serikali.
Kupitia ushirikiano huo, serikali za Ufaransa na
Canada zingetoa msaada katika mradi huo kwa mkopo nafuu lakini zikitaka
kampuni za kusambaza mashine hizo zitoke katika moja ya nchi hizo mbili.
Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la The Citizen
umeonyesha kuwa mpango huo ungegharimu Sh138.6 bilioni tofauti na
Sh146.8 bilioni ambazo Tume imepanga kutumia katika mradi huo.
Kuhusu lawama za kwa nini Nec isitumie
vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (Nida), Jaji Lubuva alisema vitambulisho hivyo havijagawiwa katika
maeneo yote nchini.
“Tutakapofika mahali, kila tunapokwenda kuna
vitambulisho vya uraia, ndipo tutaweza kuvitumia wakati wa uandikishaji
kwa kuwa vitatupa facts (taarifa) zote za mpigakura,” alisema.
Hata hivyo, alisema Katiba na sheria hairuhusu
kazi ya uandikishaji wapigakura kufanywa na Nida... “Sheria inasema kuwa
kazi ya upigaji kura itafanywa na Nec.”
Jaji Lubuva alisema vitambulisho vya Taifa
vitakapoenea, mpigakura hatakuwa tena akiulizwa kitambulisho cha
mpigakura, bali atatakiwa kutoa kitambulisho cha uraia.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip
Mangula alisema kuna mkanganyiko kati ya Mwenyekiti wa Nec na Jaji
Werema kuhusu tarehe ya kufanyika kura ya maoni.
Alitaka kusahihishwa kwa kauli hizo mbili ili kuepuka mgongano kutokana na kutofautiana huko.
Hali hiyo, ilimfanya Jaji Lubuva kurudia kwa mara nyingine kusema kuwa kura ya maoni itakuwa baada ya Machi 30 mwakani.
Alisema katika Uchaguzi Mkuu wa 2010, walitumia daftari ambalo
lilitumika mwaka 2004, ambalo lililalamikiwa na wananchi kuwa lina
kasoro nyingi hivyo uchaguzi ujao Tume yake itatumia BVR.
Jaji Lubuva alisema mfumo huo unajumuisha kamera na unamtambua mpigakura, hivyo kuondoa hofu ya mtu kuandikishwa mara mbili.
“Akija mtu ambaye ameandikishwa mahali pengine
system (mtandao) inakataa. Vijana wote waliofikia kuandikishwa
wataandikishwa na mfumo huu ndiyo utakaotupa uhakika zaidi,” alisema
Jaji Lubuva.
Alisema mfumo huo wa BVR umetumika katika nchi
nyingi za Afrika, Ghana, Liberia, Nigeria, Zambia, Afrika Kusini na
Kenya na hata Zanzibar inautumia baada ya kuingia katika serikali ya
Umoja wa Kitaifa.
“Watanzania wasione kitu cha ajabu sana, sisi
tumechelewa. Halafu sisi tutatumia mfumo huu kwa kuandikisha tu na si
ile wanayoita E voting (kupiga kura kwa mtandao),” alisema.
Alisema Kenya haikutumia mfumo huo katika kuandikisha pekee, bali na katika kusafirisha takwimu tofauti na Tanzania ambayo itatumia katika uandikishaji tu.
Source:Mwananchi.
Alisema Kenya haikutumia mfumo huo katika kuandikisha pekee, bali na katika kusafirisha takwimu tofauti na Tanzania ambayo itatumia katika uandikishaji tu.
Source:Mwananchi.
0 comments:
Post a Comment