Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye
amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho
hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali
wa vikao husika.
Nape ameyasema hayo jana kwenye
mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika
Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na
uhusiano wa CCM katika jamii.
Pamoja na Nape ambaye aliwakilisha
CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama
vingine vya upinzani nchini.
Akizungumzia mada ya nafasi na
uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho
ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au
kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini
Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo
Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa
taifa.
Nape alisema CCM ipo kila kona ya
nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo
ndio moja ya siri za uimara wa CCM.
Akizungumzia swala la maadili Nape
alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora
zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema
mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi
nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.
Alisema Nape kuwa wasaka urais
wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza
muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.
Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba
wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri
wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni
kukaribisha laana kwa nchi.
” Nawahakikishia kuwa hakuna
mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna
hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini
tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii” alisisitiza
Nape.
Nape alisema mwanzoni mwa mwaka
huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya
za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia
maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha
nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.
Anasema Nape hakuna atakayeingia
madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila
kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za
kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa
laana kwa nchi.
Semina hiyo inayofanyika Kibaha
mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa
huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini
Kenya.
HABARI KAIKA PICHA
HABARI KAIKA PICHA
MTUME na Nabii wa Kanisa la
EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu
nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya
wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea
Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa mada kwenye semina hiyo
Nape akifafanua jambokuhusu CCM ilivyo imara licha ya kuwa na mapungufu kama Taasisi kubwa
“Hili Chama ni kubwa sana, siyo
rahisi kuling’oa madarakani, ukiona unakereka a mambo ingia humohumo
ndai ya Chama ukisafishe… hiyo ndiyo dawa”, akisema Nape kwenye Semina
hiyo
“Hatukatai kwamba CCM haina
mapungufu, inayo lakini mifumo yake ni mizuri kuliko Chama chochote
Afrika na pengine duniani kote”, alisema Nape kweny Semina hiyo.
Nabii Mwingira na Mkewe wakimsikiliza Nape kwa makini wakati akitiririka kwenye utoaji mada kwenye semina hiyo
Washiriki katika semina wakifuatilia kwa makini wakati Nape akitoa mada kwenye semina hiyo
“Katiba hii ya CCM imesheheni kila kitu.. tatizo ni baadhi ya watu kusuasua katika kuyatekeleza” anasema Nape.
Nape akimaliza kutoa mada yake
kwa kuwaomba watanzania kuhakikisha nchi inapata mgombea wa Urais aliye
bora na siyo kwenye kuinunua nafasi hiyo muhimu
Nape akirejea kuketi baada ya kutoa mada kwa zaidi ya saa moja na nusu kwenye semina hiyo
Washiriki wakimshangilia Nape baada ya mada yake
Mtume na Nabii Mwingira akitoa maelezo kusadifu maneno aliyotoa Nape katika mada yake.
Waumini wakiombea Tanzania, CCM na Nape kudumu katika mwendendo ulio bora kwa manufaa ya Taifa la Tanzania
Nape akiwa amesimama wakati wa maombi hayo
Nape akienda kukutana na Mwingira kwa ajili ya kuagana baada ya semina
“Kijana umetoa mada nzuri, Mungu
amekuonyesha njia, umezungumza na kujibu maswali vema” Mwingira
akimwambia Nape wakati akimsindikiza ktoka ukumbini
Mtume na Nabii Mwingira
akimsindikiza Nape huku wakionyesha kuwa wenye furaha kwa tukio
lililotokea la CCM kushiriki kutoa mada kwenye semina hiyo
Mwingira akimsindikiza Nape hadi nje ya ukumbi
Mwingira na Nape wakiingia jengo la Utawala la EFATHA, kwa ajili ya kuagana rasmi. Picha zote na Bashir Nkoromo
0 comments:
Post a Comment