KRIKETI :TANZANIA,NAMIBIA KUCHUANA!!

Mchezaji wa Kriketi akiwa mazoezini
Wakati mashindano ya mchezo wa Kriketi yakitarajiwa kufanyika hivi karibuni, Wenyeji Tanzania wakitarajiwakucheza na Namibia katika mechi ya ufunguzi wa mashindano yaho ya Afrika kwa vijana wa kiume wenye umri chini ya miaka 19 itakayochezwa katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam Jumamosi ya February 14.
Wachezaji wa Tanzania wanafanya mazoezi Dar es Salaam wakiwa chini ya kocha mchezaji, Hamis Abdallah.
Michuano hiyo ya Juma moja itakuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza kombe la dunia la vijana chini ya miaka 19 litakalofanyika, Dhaka, Bangladesh mwakani.
Timu nyingine Shiriki za michuno hiyo kufuzu zitatoka katika nchi za Namibia, Nigeria, Botswana, Kenya na Uganda na zinategemewa kuwasili Dar es Salaam siku mbili kabla ya mashindano.
Kocha Abdallah, aliyewahi kucheza kriketi katika Klabu ya Watford Town ya Uingereza kwa miaka kadhaa, amesema atachagua timu yake ya mwisho baada ya mechi za majaribio zitakazochezwa wikiendi hii.
''Kwa sasa nina kikosi (provisional squad) cha wachezaji zaidi ya 20 kambini, nitachagua timu ya wachezaji 12 ambao ndio watakuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano hiyo”, amesema Abdalllah, aliyesomea ukocha na ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya wakubwa.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment