Nigeria inachunguza taarifa za
ubakaji, usafirishaji wa watoto na udhalilishaji mwingine katika kambi
za watu wanaokimbia mashambulio ya wapiganaji wa Kiislam wa kundi la
Boko Haram.
Msemaji wa Nema ameiambia BBC kuwa wachunguzi watatembelea kila kambi ya watu waliokimbia makazi yao.
Watu wapatao milioni 3.2 raia wa Nigeria wameyakimbia makazi yao kuwakimbia wapiganaji wa Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Uchunguzi wa shirika la Nema ni matokeo ya ripoti iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Taarifa za Uchunguzi lenye makao yake Calabar Nigeria(ICIR).
0 comments:
Post a Comment