Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chauka), Hassan Mchanjama (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar. |
Mwenyekiti wa Chakua, Hassan Mchanjama alisema
mafuta yamepungua bei kutoka Sh2,200 hadi Sh1,768 kwa lita moja ya
petroli huku diseli ikishuka hadi kufikia Sh1,708 kwa lita.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo, Mchanjama alisema wanapendekeza nauli ishuke kwa
asilimia 25 kwa usafiri wa daladala inayoenda masafa ya chini ya
kilometa 10.
Alifafanua kuwa kwa nauli ya sasa ya Sh400,
kushuka kwa bei ya mafuta kutafanya nauli pia ishuke hadi kufikia Sh300
na kwa upande wa mabasi ya mikoani nauli ishuke kutoka Sh40,000 hadi
Sh30,000.
Alifafanua kuwa kushuka kwa nauli za mabasi
kutasababisha pia kushuka kwa bei ya bidhaa mbalimbali ikiwemo chakula
na mazao mengine ya biashara.
Chama hicho kimemuomba pia Waziri wa Uchukuzi,
Samweli Sitta aingilie kati na kuiagiza Sumatra isikilize kilio cha
wananchi kwa kuitisha mkutano ili kushusha nauli kama ilivyokuwa mwaka
2009 baada ya mafuta kupungua bei nauli zikapungua.
0 comments:
Post a Comment