Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe akiwa pamoja na Mbunge Joshua Nassari (kushoto) na Godbless Lema (kulia) katika moja ya mikutano ya chama hicho. Picha na Maktaba |
Majimbo hayo ni jimbo la Arusha mjini, mbunge
wake, Godbless Lema, Jimbo la Arumeru Mashariki, mbunge Joshua Nassari
na Jimbo la Karatu mbunge, Mchungaji Israel Natse ambapo tayari kuna
wanachama wa chama hicho, wameanza kutangaza nia za kuwang’oa
wabunge hao.
Akizungumza na mwandishi wetu leo, Katibu wa Chadema
mkoa wa Arusha, Calist Lazaro alisema, maagizo anayoyatoa ni kutekeleza
utaratibu ambao umetolewa na Kamati Kuu ya chama hicho,kuhusiana na
uchaguzi mkuu ujao.
“Naomba hapa ieleweke kuwa hatuzuwii mtu kugombea
lakini tunataka afuate taratibu ili kuzuia vurugu na kama mtu akikiuka
sasa ina maana atakuwa amepoteza sifa”alisema Lazaro.
Lazaro alisema nia ya agizo hilo ni kuondoa vurugu
na mpasuko ndani ya chama kabla ya wakati muafaka wa kutangaza nia na
kuanza kampeni haujafika, lakini kwa majimbo yaliyo na wabunge wa CCM,
wagombea wanaruhusiwa kutangaza nia.
Alisema chama hicho, kitatoa ratiba ya uchaguzi
karibuni na fomu za kugombea nafasi mbali mbali zitapatikana katika
ofisi za chama hicho, katika ngazi zote ila kwa maeneo yenye wabunge na
madiwani wa chadema, fomu zitapokelewa bila kutangaza nia na kuanza
kampeni.
Tamko hilo limekuja kukiwa na mpasuko mkubwa ndani
ya Chadema katika majimbo hayo matatu, kutokana na idadi kubwa ya
makada wa chama hicho, kuanza kunyemelea majimbo hayo.
0 comments:
Post a Comment