WAANGALIZI ZAIDI WA MUUNGANO WA ULAYA WAWASILI TANZANIA!!

Waangalizi wa muda mfupi kutoka Muungano wa Ulaya  wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.

Waangalizi hao 60 waliwasili jijini Dar es Salaam jana na wanatarajiwa kutumwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuanzia Jumanne.

Hatahivyo waangalizi hao wataungana na waangalizi wa muda mrefu wa muungano huo ambao wamekuwa wakifuatilia maandalizi ya uchaguzi pamoja na kampeni tangu mwisho wa mwezi Septemba.

Waangalizi hao wa muda mfupi wanafikisha 140, jumla ya waangalizi waliotumwa na Muungano wa Ulaya kuangalia uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara tuu baada yakutua kwenye uwanja wa ndege mjini Dar res salaam jana mmoja wa waangaluzi hao alisema
"Tutakuwa na waangalizi 140 watakaotembelea vituo vya kupiga kura kwenye maeneo ya mijini na vijijini, kwenye
Mikoa yote, ili kuangalia upigaji na kuhesabiwa kwa kura,” amesema Mwangalizi Mkuu wa EU, Judith Sargentini.
“Waangalizi wetu watafuatilia pia uorodheshwaji wa matokeo, ambazo ni sehemu muhimu ya tathmini ya jumla ya EU EOM ya mchakato wa uchaguzi.”

Waangalizi hao wa uchaguzi watakuwa nchini Tanzania hadi Novemba 15 na wanatarajiwa kutoa tathmini ya awali kuhusu uchaguzi huo muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wenyewe.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment