VIJANA WA VYUO VIKUU NA WASOMI WAKUTANA MKOANI DODOMA KUZUNGUMZIA MASUALA YA VIJANA NA KUJITAMBUA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU!!


Mkuu wa wilaya ya Dodoma Dokta Jasmin Tiisikwe amewataka vijana hususani wasomi kujitofautisha na vijana wa mtaani ambao wanashindwa kupangilia hoja kwani kwa kushindwa kufanya hivyo jamii itashindwa kuwatofautisha na kukosa maana kamili ya wasomi na wale wasio wasomi na kufanya maamuzi ya mabadiliko ya kweli na siyo mabadiliko ya kulididimiza Taifa.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kongamano la vijana lililowahusisha wanavyuo wa mkoa wa Dodoma katika ukumbi wa Lands Mack ulioko kilimani mkoani hapa akiwa ni mgeni rasmi ambapo aliungana na vijana pamoja na wapenda Amani mkoani Dodoma kujadili juu ya mustakabali wa nchi kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Hata hivyo mkuu huyo amewataka vijana hao wa vyuo vikuu Dodoma kutumia ujuzi wao katika kutetea Amani na kuleta umoja pamoja na misingi mingine aliyoiacha muasisi wa taifa hili.

Nae alex sanga kutoka chuo kikuu cha saint john’s mkoani hapa amesema kuwa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu vijana wanapaswa kuondokana na fikra potofu kuwa kutakuwepo na machafuko hivyo kila raia anapaswa kuweka baadhi ya mahitaji ya kutosha ndani katika kipindi hiki jambo ambalo ni uzushi na nchi hii itaendelea kuwa na Amani kama kawaida hata baada ya uchaguzi.

Wakichangia katika kongamano hilo baadhi ya vijana wametoa   maoni yao juu ya mbinu na mambo yanayotakiwa kuzingatiwa kabla na baada ya uchaguzi.
Tazama picha nyinginezo hapa
   










































Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment