Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ,jijini Dares Salaam.
" Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza uzalishaji na hatimaye kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini ," alisema Balozi Seif.
Aliongeza kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya kuendeleza vijana.
" Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina dhamira ya Kuimarisha viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha vijana kupata ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi za maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao," alisisitiza.
Aidha aliongeza kwamba kupitia chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine la wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi amabo ni milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana na Sera ya Wazee kundi hilo linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na huduma nyingine muhimu.
"Serikali na wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali ya uchumi wan chi," alisema.
Balozi Seif alizita Wizara ,Idara na Taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha sera zilizopo na kutumia takwimu hizi katika kupanga mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk. Albina Chuwa alisema chapisho hilo linaonesha kuwa umri unaoanzia miaka 0 hadi 4 kuashiria kuwa kiwango cha uzazi bado ni kikubwa.
Alifafanua kuwa kwamujibu wa Utafiti wa Mama na Mtoto wa mwaka 2010 kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa miaka 15hadi 49, hivyo uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia (UNFPA)Mariam Khan alisema chapisho hilo litasaidia kujua iddai ya watu wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga uzazi wa mpango na mipango mingineyo.
0 comments:
Post a Comment