WAHAMIAJI HARAMU 18 KUTOKA ETHIOPIA WAKAMATWA KILIMANJARO...

 
WAHAMIAJI haramu wapatao 18 wote raia wa Ethiopia,wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa njiani kusafirishwa kwenda mikoa ya kusini na baadaye kuvuka mpaka wa Tanzania kwenda Afrika Kusini.

Wengi wa wahamiaji hao haramu ni vijana wenye umri wa miaka kati ya miaka 20 na 27 ambao walikamatwa majira ya saa 6:30 usiku wa kuamkia leo wakiwa ndani ya gari lenye namba za usajaili T858AHW likiwa na tela lake lenye namba za usajili T419AAE mali ya kampuni ya SUNVIC ya Jijini Arusha.

Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule amesema wahamiaji hao haramu walikamatwa katika eneo la Kichwa ng’ombe wilayani Mwanga kwa ushirikiano na maofisa wa uhamiaji na askari wa jeshi la polisi.

Alisema baada ya kukamatwa kwa gari hilo dereva alifanikiwa kuchomoa funguo wa gari na kisha kukimbia kusikojulikana na kuamua kulitelekeza gari hilo katika eneo la Kifaru,hata hivyo  juhudi za kumtafuta dereva huyo zinaendelea.

Msumule alisema kutokana na kitendo hicho cha dereva kukimbia na funguo wa gari hilo,Maofisa wa uhamiaji walilazimika kuwasiliana na wamiliki wa gari ambao ni kampuni ya SUNVIC ndipo walipowapatia funguo nyingine.

“Baada ya dereva wa gari kukimbia na funguo tulishindwa kuliondoa katika eneo la tukio ndipo tukawasiliana na kampuni inayomiliki Lori hilo iliyoko jijini Arusha ambao walitupatia ushirikiano mkubwa ,hatimaye mchana walituletea funguzo za gari hilo.”alisema Msumule.

Msumule alitoa onyo kwa wahamiaji haramu pamoja na wale wanao wasaidia ikiwa ni pamoja na kuwasafirisha pamoja na kuwahifadhi kuwa idara yake imejipanga vyema kukomesha biashara hiyo.

“Kama nilivyozungumza hapo siku za mwanzo,tunataka biashara hii katika mkoa weru wa Kilimanjaro ifutike kabisa,hatuna utani na hatutaki mtu achezee shughuli hii tunayoenda kuifanya “alisema Msumule.

 
Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Mwanga wakiwa chini ya ulinzi mara baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi.

Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Mwanga wakiwa katika gari la Polisi wakifikishwa makao makuu ya uhamiaji ya mkoa wa Kilimamnjaro mjini Moshi

Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Mwanga wakishuka kutoka kwenye landrover ya Polisi mara baaba yakufikishwa katika ofisi za Uhamiaji Mkoa Kilimanjaro.

Wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia waliokamatwa eneo la Mwanga  wakitokea nchini Kenya.

Mmoja wa wahamiaji haramu raia wa Ethiopia aliyafahamika kwa jina la Jamal Amir akilia kwa uchungu baada ya kukamatwa na maofisa wa uhamiaji katika eneo la Mwanga.

 

Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule akizungumza mara baada ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu 18 kutoka nchini Ethiopia.

Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule akizungumza jambo na mmoja wa wahamiaji haramu aliyefahamika kwa jina la Jamal Amir mara baada ya kukamatwa wakiingia nchini bila kufuata taratibu.

Baadhi ya wahamiaji haramu wakilia kwa uchungu mara baada ya kukamatwa wakiingia nchini bila kufuata taratibu.

Wahamiaji haramu wakienda kunawa mikono na kipata chakula kilichotolewa na ofisi ya uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro baada ya wengi wao kuonekana kudhoofika kutokana na kukosa chakula kwa muda mrefu.

Wahamiaji haramu wakipata chakula
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment