KWENYE Mechi pekee ya BPL, Ligi Kuu
England, Jana Usiku Fulham waliichapa Crystal Palace Bao 4-1 na
Wachezaji wao Pajtim Kasami na Steve Sidwell kufunga Bao 2 safi sana
ambazo, bila shaka, zimo kwenye kinyang’anyiro cha Goli la Msimu.
Adrian Mariappa ndie aliwapa Crystal
Palace bao lao pekee kwa kichwa lakini Kasami na Sidwell wakaigeuza
Mechi hiyo kabla ya Haftaimu.
Kipindi cha Pili, kichwa cha Dimitar Berbatov na tikitaka ya Philippe Senderos kiliwapa Fulham ushindi mnono.
Magoli:
Crystal Palace 1
-Mariappa Dakika ya 7
Fulham 4
-Kasami Dakika ya 19
-Sidwell 45
-Berbatov 50
-Senderos 55
Hiki
ni kipigo cha 7 kwa Crystal Palace katika Mechi zao8 za Ligi na wapo
Nafasi ya 19 ikiwa ni Nafasi moja toka mkiani na hii ni presha kubwa kwa
Meneja wao Ian Holloway.
Kwa Fulham, huu ni ushindi wao wa pili
mfululizo kwenye Ligi na umewapandisha hadi Nafasi ya 14 na kumpa ahueni
Meneja wao Martin Jol aliekuwa akisakamwa.
Jose Mourinho: afunguliwa Mashitaka na FA
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho
amefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa utovu wa
Nidhamu kwenye Mechi ya ushindi wa Klabu yake walipoichapa Cardiff City
Bao 4-1 Jumamosi iliyopita Uwanjani Stamford Bridge.
Kwenye Mechi hiyo, Refa Anthony Taylor
alimwondoa Mourinho toka kwenye Benchi la Ufundi baada ya kulalamikia
upotezaji muda waa Wachezaji wa Cardiff City na Meneja huyo akalazimika
kuitazama Mechi hiyo kwa Dakika 20 zilizobaki akiwa Jukwaa la Washabiki.
Kabla kufunguliwa Mashitaka, Mourinho alisema: “Sielewi kwa nini Refa amenizuia kufanya kazi yangu!”
Mbali ya Mourinho kupewa Kadi Nyekundu,
pia kwenye Mechi hiyo kulikuwa na utata mkubwa pale Bao la kusawazisha
la Chelsea kukubaliwa kinyume na Sheria za FIFA kwani Kipa wa Crystal
Palace Marshall alikuwa ameudaka Mpira na aliudunda chini na Eto’o
kuudokoa na baadae kumfikia Hazard aliefunga.
Kwa mujibu wa FIFA, tukio hilo lilipaswa kuamuliwa ni faulo dhidi ya Chelsea.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment