Sir
Alex Ferguson leo amezindua Kitabu cha maisha yake na miongoni mwa
mengi yaliyoibuliwa humo ni sababu zilizofanya David Beckham kuondoka
Manchester United.
Katika Kitabu hicho kiitwacho ‘Alex Ferguson: My Autobiography’,
Ferguson amesema ilifika hatua Beckham kujiona ‘yu mkubwa kupita
Meneja!’ na walianza kukorofishana wakati Beckham alipopondwa kwa
kucheza vibaya wakati Man United ilipofungwa na Arsenal Mwaka 2003
kwenye FA CUP.
Ferguson ameeleza: “Ikifika Dakika
Mchezaji wa Manchester United anajiona yuko mkubwa kupita Meneja, lazima
aondoke. David alijiona yu mkubwa kupita Alex Ferguson.”
MAMBO MUHIMU YANAYOELEZEWA HUMO:
-Wayne Rooney alipoteza ukali wake Msimu uliopita ambao ndio ulikuwa wa mwisho kwa Ferguson kwa kuwa hakuwa fiti.
-Aliigomea England mara mbili kuwa Meneja wake
-Cristiano Ronaldo ndie Mchezaji mwenye Kipaji kikubwa kupita yeyote aliewahi kumwongoza na anamuita ‘Mchawi.’
-Alimwambia Ronaldo yuko tayari kumpiga risasi kuliko kumuuza kwa Real Madrid
-Kitu kigumu katika mwili wa Roy Keane ni ulimi wake na alikuwa na kauli mbaya kupita mfano!
-England hawawezi kutwaa Kombe la Dunia mpaka wapate Wachezaji wenye kipaji kama Brazil
Ferguson pia ameandika kuwa alikerwa na
maisha ya Beckham ya kusaka umaarufu baada ya kumuoa Mwimbaji wa Kundi
la Spice Girls Victoria Adams.
Ferguson amesema: “David alikuwa ndie
Mchezaji pekee niliemwongoza aliechagua umaarufu, alietaka kujulikana
nje ya Gemu. Sikusikia vizuri na maisha hayo ya umaarufu.”
Beckham, ambae akiwa na Man United
alinyakua Ubingwa wa Ligi mara 6, FA CUP 2 na UEFA CHAMPIONZ LIGI moja,
aliuzwa kwa Real Madrid Mawaka 2003 kwa Pauni Milioni 25.
Katika Miaka yake 26 akiwa na Man
United, Sir Alex Ferguson alitwaa Makombe 38 na kuongoza baadhi ya
Majina makubwa kwenye Soka wakiwemo Beckham, Eric Cantona, Cristiano
Ronaldo, Peter Schmeichel, Bryan Robson, Roy Keane, Jaap Stam na Ruud
Van Nistelrooy.
Ferguson alistaafu Man United Mwezi Mei na nafasi yake kuchukuliwa na David Moyes alietokea Everton.
POSTED BY:www.info@dirayetu.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment