MWANAHARAKATI WA KUGOMBEA HAKI ZA MTOTO WA KIKE KUTOKA MAREKANI ATUA DAR.

 Zuriel Oduwole, msichana mdogo wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, yupo jijini Dar es salaam hivi tunavyoongea akiwa na wazazi wake na wadogo zake watatu, katika harakati zake za kutoa elimu juu ya umuhimu wa kumuendeleza mtoto wa kike katika Afrika. 

Tayari Zuriel ameshafanya mahojiano na Marais wanane (akiwemo Rais Kikwete) pamoja na Waziri Mkuu wanne wa Afrika, pamoja na mfanyabiashara tajiri kuliko wote Afrika Bw. Dangote, hali kadhalika nyota wa tennis duniani toka Marekani, Venus na Serena Williams.
Zuriel, ambaye ni mtengezea filamu, mwanahabari na mwanaharakati wa maslahi ya wasishana wadogo,  yuko nchini akitokea Malawi ambako kama ilivyokuwa hako, hapa nchini, hususan jijini Dar es salaam, atafanya mihadhara katika shule kadhaa ya kuhamasisha wasichana wadogo wajiamini na kusaidia katika kuzungusha gurumu la maendeleo huku wakipiga vita unyanyapaa dhidi yao. Mwezi Agosti mwaka huu Zureil aliweka historia ya kuwa mtu mwenye umri mdogo kuliko wote waliopata kuhojiwa na jarida maarufu la watu maarufu na matajiri duniani la Forbes. VHapideo ya hapo chini kabisa ni moja ya vipindi alivyoandaa:
 Zureil akimhoji Rais wa Liberia Mhe Mama Ellen Johnson Sirleaf
 Zureil akimhoji Rais wa Nigerai Mhe Goodluck Jonathan
 Zureil akimhoji Mhe Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Zureil akimhoji Rais wa Cape Verde Mhe Jorge Carlos Fonseca
Zuriel akiongea na Rais Jakaya Kikwete
Zuriel akimhoji Rais wa Sudan ya Kusini Mhe Salva Kiir Mayardit.      
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment