WENGER ASEMA MAN UNITED BADO WAMO KATIKA MBIO ZA UBINGWA!!

                                                                                                                                                                   WENGER: ‘WANAO WACHEZAJI WAKUBWA, UZOEFU MKUBWA NA NI KLABU KUBWA!’

MAN_UNITED-2013-TROPHYMENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Mabingwa Manchester United bado wamo kwenye mbio za kuwania Ubingwa wa England licha ya kuwa Timu yake ipo kileleni mwa BPL, Ligi Kuu England, Pointi 8 mbele ya Man United.

Baada ya Mechi 8, Man United wapo Nafasi ya 8 na huu ni mwanzo mbovu kabisa kwao kwenye Ligi katika Miaka 24.
Wenger amesema: “Je Man United wako nje ya mbio za Ubingwa? Hapana, lakini ingekuwa Pointi 10 lingekuwa ni pengo kubwa kidogo!”
Aliongeza: “Wao wana Wachezaji wakubwa, wenye uzoefu mkubwa na ni Klabu kubwa!”
Juzi Jumamosi, Bao la Dakika ya 89 la Adam Lallana wa Southampton liliwanyima Man United ushindi walipotoka Sare 1-1 na Southampton kwenye Mechi ya Ligi iliyochezwa Uwanjani Old Trafford.
Siku hiyo hiyo, Arsenal waliitwanga Norwich City Bao 4-1 na kukaa kileleni wakiwa Pointi 2 mbele ya Chelsea.
Wenger ametamka: “Ukiwa na chaguo, utataka uwe kwenye mbio juu kileleni, lakini leo hii huwezi kuwaondoa Man United! Ni mapema mno! Ni gemu 3 tu na Msimamo unabadilika!”
Man United walianza Ligi kwa kuichapa Swansea Bao 4-1 na wametoka Sare mbili na Chelsea na Southampton kuzifunga Sunderland na Crystal Palace lakini wamefungwa na Liverpool, Manchester City na West Brom.
BPL: LIGI KUU ENGLAND
[Saa za Bongo]
Jumatatu 21 Oktoba
22:00 Crystal Palace v Fulham
Jumamosi 26 Oktoba
14:45 Crystal Palace v Arsenal
17:00 Aston Villa v Everton
17:00 Liverpool v West Bromwich Albion
17:00 Manchester United v Stoke City
17:00 Norwich City v Cardiff City
19:30 Southampton v Fulham
Jumapili 27 Oktoba
1630 Sunderland v Newcastle United
1900 Chelsea v Manchester City
19:00 Swansea City v West Ham United
10:00 Tottenham Hotspur v Hull City
[Hata hivyo inasemekana huenda Majira huko England yakabadilika kuanzia Jumapili Oktoba 27]

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
8
9
19
2
Chelsea
8
9
17
3
Liverpool
8
6
17
4
Man City
8
11
16
5
Tottenham
8
3
16
6
Southampton
8
5
15
7
Everton
8
2
15
8
Man Utd
8
1
11
9
Hull
8
-2
11
10
Newcastle
8
-3
11
11
Swansea
8
1
10
12
West Brom
8
1
10
13
Aston Villa
8
-1
10
14
West Ham
8
0
8
15
Stoke
8
-3
8
16
Cardiff
8
-5
8
17
Fulham
7
-4
7
18
Norwich
8
-7
7
19
Crystal Palace
7
-8
3
20
Sunderland
8
-15
1
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment