Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akipongezwa na Mkurugenzi
Msaidizi wa Wanyamapori Paul Sarakikya mara baada ya kumaliza mahojiano
katika kituo cha BBC jijini London alipokuwa akihudhuria Mkutano wa
Kimataifa wa Biashara Haramu ya Wanyamapori. Kulia ni Katibu wa Waziri
Imani Nkuwi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) alipata fursa ya
kukutana na Mwandishi wa Gazeti la Daily Mail la Nchini Uingereza Martin
Fletcher (kulia) na kumfafanulia juu ya juhudi za serikali katika
kupambana na ujangili nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Wanyamapori Paul Sarakikya.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akihojiwa na Mtangazaji
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) Zawadi Machibya ambapo alipata
nafasi ya kuzungumzia juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika
Vita Dhidi ya Ujangili nchini na Changamoto zinazohitaji kuungwa mkono
na Jumuiya ya Kimataifa.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe.
James Lembeli (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Wanyamapori
Paul Sarakikya (kulia) jijini London walipohudhuria Mkutano wa
Kimataifa wa Biashara Haramu ya Wanyamapori. Kati ni Katibu wa Waziri
Imani Nkuwi.Picha na Pascal Shelutete, TANAPA
0 comments:
Post a Comment