Akizungumza na gazeti
hili jana akiwa njiani kuelekea Dodoma kushiriki Kikao cha Bunge la
Katiba, Lema alisema maafisa wawili wa polisi walimfuata katika hoteli
aliyofikia Dar es Salaam kwa lengo la kumkamata na kumpeleka makao makuu
ya polisi.
Lema alisema maafisa hao, ambao walikuwa
wanatumia gari dogo, baada ya kufika hotelini hapo, waliomba aitwe na
aliposhuka walimtaka kuandamana nao, hadi makao makuu ya polisi kwa
mahojiano.
“Niliwauliza nikaandeke maelezo juu ya nini,
walijibu kifupi wao ni chombo cha dola na walisema wametumwa na viongozi
wa juu wa polisi na hawakuwa tayari kutaja tuhuma zangu,” alisema Lema.
Alisema baada ya polisi hao kusisitiza kutaka kumchukua,
aliwaomba aende chumbani kujiandaa kabla ya kuwasiliana na viongozi wa
chama chake na familia yake.
“Niliposhuka chini sikuwakuta
na ndipo nikashauriana na viongozi wa chama hicho na kuamua kuondoka
jana mchana Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
Hata hivyo,
alisema Chadema leo wanatarajia kutoa tamko juu ya kauli ya Rais Jakaya
Kikwete kuwataka wanachama wa CCM kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani
hasa pale wanapodaiwa kupigwa.MWANANCHI
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment