WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE WAPIGWA MSASA JUU YA WELEDI WA KURIPOTI HABARI ZA BUNGE!!

 

Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Jossey Mwakasyuka (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari kuhusu kuimarisha Uandishi wa Habari za shughuli za Bunge iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma. Kulia ni Mshauri wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna Kochannesyan.
Mhariri Mtendaji Jamhuri Media Limited, Bw. Deodatus Balile akitoa mada mbele ya waandishi wa habari (hawako pichani) inayohusu Athari za Siasa katika uandishi wa Habari za Bunge, Madhara ya Vyombo vya habari kutumika, Miiko na Maadili ya kuzingatia wakati wa semina kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Bw. Athumani Hussein akitoa mada inayohusu Uandishi wa habari za Bunge na Siasa wenye tija kwa Taifa wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Mshauri wa mambo ya Kiufundi toka Shirika la UNDP, Bi. Anna Kochannesyan akichangia mada wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Afisa Habari wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Owen Mwandumbya akifafanua jambo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini mada zikizowasilishwa wakati wa semina iliyoandaliwa leo kwa ajili yao iliyofanyika tarehe 6 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa African Dreams Conference mjini Dodoma.


WAANDISHI wa habari nchini wameaaswa kuandika habari zinazohusiana na masuala ya Bunge, likiwemo Bunge Maalum la Katiba kwa kuzingatia weledi na kujiepusha kuwa na maslahi binasfi au ya kisiasa.

Hayo yalisemwa leo 6 Septemba, 2014 na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Jamhuri , Deodatus Balile wakati wa semina kuhusu namna bora ya kuimarisha uandishi wa habari za shughuli za Bunge iliyofanyika kwenye hoteli ya African Dreams mjini Dodoma.

Akizungumza awali kabla ya kuanza kwa Semina hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Habari ya Bunge kwa kushirikana na Shirika la UNDP, Mkurugenzi wa Habari, Elimu kwa Umma na Itifaki wa Bunge Maalum, Bw. Jossey Mwakasyuka amesema lengo lake ni kuweza kujadiliana na kubadilishana uzoefu juu ya uandishi wa habari hizo kwa waandishi hao ili kuweza kuandika habari sahihi.

Balile amesema hayo wakati akitoa mada kuhus u Athari za kisiasa katika uandishi wa habari wa Bunge , Madhara ya Vyombo vya Habari kutumika, miiko na maadili ya kuzingatia kwenye uandishi wa habari hizo.

“Ni lazima kutenganisha uandishi wa habari na siasa, ikiwa kama unataka kuingia katika siasa basi inapaswa kuacha kazi ya uandishi wa habari,” alisema Balile.

Aidha, Balile amewataka waandishi wa habari kujiepusha kuandika habari zinazohusu siasa na Bunge ambazo zinajenga chuki katika jamii, ikiwemo kuiingiza hisia binafsi ama upendeleo.

“Ni vema habari zinazohusu maendeleo, umoja mshikamano na zenye kuleta amani zipewe kipaumbele,” alisisitiza Balile. Aliongeza kuwa ni vema waandishi hao wakajenga tabia ya kujiendeleza kielimu katika fani mbalimbali ili kuweza kufanya kazi hiyo kiufasaha na kujiheshimu kwani wakijiheshimu nao wataheshimiwa,huku akiwapongeza baadhi yao ambao wamejiendeleza au wanajiendeleza kielimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Kamati za Bunge Maalum, Athuman Hussein, akitoa mada kuhusu Uandishi wa Habari za Kibunge wenye Tija kwa Taifa amewataka waandishi hao kuweza kukumbuka mara kwa mara mambo ambayo yatasaidia kuongeza ufanisi katika kazi zao.

“Unapoandika habari za Bunge ni lazima uwe na uelewa wa matarajio ya wananchi ili uweze kuandika habari zenye tija. Huwezi kuandika habari zenye tija kama hujui matarajio ya wananchi,” alisema Hussein.

Hussein aliongeza kuwa na uelewa juu ya Bunge na majukumu yake, muundo wake na mifumo yake ni jambo muhimu kwa waandishi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment